23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Dk. Tulia alaani kaburi kufukuliwa

Na ELIUD NGONDO, MBEYA

NAIBU Spika, Dk. Tulia Ackson amelaani vikali matukio ya kufukuliwa miili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) mkoani Mbeya kuwa hayatavumiliwa, kwani ni kuunyanyasa mwili.

Hayo amezungumza wiki iliyopita na  waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mashindano ya Tulia Marathon yatakayofanyika mkoani  hapa Mei 4, mwaka huu.

Alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya swali kutoka kwa mwandishi kuuliza juu ya kufukuliwa kwa kwa kaburi la Aman Kalyembe aliyekuwa albino ambaye alizikwa mwaka 2015 na kufukuliwa usiku wa kuamkia Aprili 23, mwaka huu katika kijiji cha Ibililo kata ya Nkunga wilayani Rungwe na kuondoka nao.

Alisema watu wamekuwa na imani za kishirikina ambazo haziwezi kuwaletea maendeleo kutokana na miili ya hao Albino haina madini yoyote ni sawa na yabinadamu wengine.

“Hii hali sasa imezidi kwani hao Albino nao ni binadamu kama tulivyo wengine, hivyo kuchukua viongo vyao ni sawa na kuchukua kiungo cha binadamu yeyote ambacho hakina manufaa yoyote kwa kuongeza uchumi”, alisema Dk. Tulia.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho,Cloud Mwakyoma alisema wanaamini kuwa hawapo salama kutokana na matendo hayo kuendelea kutokea kwani kila muda wamekuwa wakisahaulika kama sio bianadamu.

“Tunaendelea kuamini kuwa hatupo salama kwasababu wakimaliza kufukua makaburi na kuondoka na miili ya marehemu wataanza kutuwinda tulio hai na kibaya zaidi mambo yanaishia Polisi huku hakuna viongozi ambao wanakemea katika mikutano yao,” alisema Mwakyoma.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakiishi pasipo kuwa na amani kwa kuhofia kuweza kutokewa na matukio kama hayo ya kutolewa uhai wao ama kuweza kukatwa baadhi ya viungo vyao na watu ambao wamekuwa wakifanya unyama huo.

Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho Mbeya Vijijini, William Simwali ambaye aliwahi kupatwa na tukio kama hilo ndani ya familia yako alisema tukio lililotokea Rungwe wanamwachia Mungu maana hawana watetezi.

Alisema yamekuwa yakitokea matukio mengi ya namna hiyo lakini kitu cha kushangaza ni kuona mambo yanafumbiwa macho kwani hakuna hata siku moja ambayo nwaliotenda hivyo kuwahi kukamatwa na kusikia wakiwa wamefungwa.

“Imefika mahali ambapo watu wenye ualbino wanashindwa kuishi kwa huru na kuweza kufanya shughuri zao kama watu wengine, hali ambayo ni hatari kubwa kwa watu wa aina hiyo”, aliongeza kusema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles