23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Dk. Tulia aiomba CRDB kuendelea kushirikiana na Bunge

Na Radhani Hassan, Dodoma

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amekabidhi zawadi kwa washindi wa
Bonanza la Michezo lilofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma huku timu ya
Bunge Sport Club ikiibuka na ushindi wa jumla katika bonanza hilo.

Akizungumza katika bonanza hilo, Naibu Spika ameiomba Benki ya CRDB
kuendeleza utamaduni ambao wamekuwa nao kila mwaka wa kushirikiana na
Bunge katika kuhamasisha michezo na kujenga mahusiano.

Akikabidhi kombe na Medali kwa Mshindi wa jumla timu ya Bunge SC
ambayo ilipokelewa na Naibu Spika, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Pauline Gekul aliwapongeza washindi katika bonanza
hilo na kuwashukuru watumishi wote wa Serikali, Bunge huku akiahidi
Serikali kuendeleza michezo nchini.

Bonanza hilo lilishirikisha michezo ya Soka,Mpira wa
Pete,Basketiball,kuvuta kamba ,Drafti kulenga shabaha, bao, kukimbia na
magunia, kufukuza kuku, mchezo wa  karata, draft, pamoja na pool
table.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles