27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa: Rasimu ni mgororo unaofukuta

Dk. Wilbrod Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa

NA ELIZABETH HOMBO, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema kupitishwa kwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa bila maridhiano ni msingi wa mgogoro unaofukuta.

Pia amewataka Watanzania wasome ibara ya 20 ya rasimu hiyo ndipo watagundua kilichofanyika.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, Dk. Slaa alisema wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wanaweza wakawa na uhalali wa kisheria, lakini hakuna maridhiano.

“Kupitisha rasimu hii bila maridhiano ni msingi wa mgogoro unaofukuta, unaweza kuwa na uhalali kisheria, lakini hakuna maridhiano.

“Ninawaomba Watanzania wasome ibara ya 20 na wasiwe mbumbumbu, Katiba ya 1977 ibara ya 6 na 7 inatoa haki ya uhai, elimu, siasa mambo ya wanawake na zote hizi hazidaiwi mahakamani, lakini kwenye rasimu hii ibara hiyo imeachwa kama ilivyo…hizi ni propaganda kwa mtu yeyote anayejua kuchambua. Kiujumla nimesikitika sana,” alisema Dk. Slaa.

Katika hatua nyingine alieleza kushangazwa na hatua ya upigaji kura kwa njia ya mtandao na wajumbe kufanya kampeni huku wakiwa wameshapiga kura.

“Sijawahi kuona mtu anapiga kura halafu wakati huo huo anafanya kampeni, mfano mjumbe anapiga kura huku anasema kwamba anawakilisha kundi fulani.

“Nimeshangaa kwa kitendo cha siku tatu kutumika kwa ajili ya kuhesabu kura wakati wajumbe hata 500 hawafiki sielewei hii tafsiri yake ni nini.

“Pia sijawahi kuona duniani kote kura kupigwa kwa njia ya fax au email kwa sababu kwa njia hizi mtu anaweza ‘akaediti’ na kuweka kile wanachokitaka,” alisema Dk. Slaa.

KAFULILA

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema kilichafanyika ni maigizo  kwa kuwa hakina mwisho.

“Katiba haiwezi kupatikana kwa utaratibu huu bila kuwapo maridhiano. Tumepoteza fedha nyingi, muda mwingi kwa kufanya maigizo tu,” alisema Kafulila.

JUSSA

Mwakilishi wa Mji Mkonge, Ismail Jussa Ladhu (CUF), alisema Bunge Maalumu la Katiba limejichanganya kuhusu namba.

“Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba anasema wajumbe kutoka Zanzibar ni 210 huku katibu wake akisema 219. Pia mjumbe wa Bunge hilo, Abdallah Abas tangu zoezi la upigaji kura lianze alitoka nje, lakini amehesababiwa,” alisema Jusa.

- Advertisement -

Related Articles

5 COMMENTS

  1. Mimi nadhani wakati umefika kwa viongozi wetu kuacha usanii, ubabe na kulazimisha mambo hata kama hayakubaliki.
    Tujenge hali ya kusikilizana, kuthaminiana na kuheshimu wengine.
    NINAIOMBEA NCHI YANGU.

  2. Haikuwa rahisi kuamini kama hawa ndugu wagefanya hicho walichofanya. CCM wanajua kuwa katiba hii ikipigiwa kura haitakubalika na wananchi. Lakini wamejipanga kugeuza kura za ndio ziwe hapana na za hapana ziwe ndio maana ni mafundi katika hilo. Baada ya hapo nchi itakosa utulivu kwa kiasi kikubwa na kuingia katika vurugu.

  3. Rais Kikwete kuwa shupavu kwa kuiweka Rasimu hii pembeni hadi
    pale maridhiano yatakapokuwepo.Umeshaonyesha nia nzuri ya kulete mabadiliko ya Katiba lakini wasiotaka maridhiano na uhitimishaji safi we awamu yako wamepitisha katiba itakayozàa migogoro.Nakuombea Mwenyezi Mungu akujaze ujasiri huo.

  4. Katiba hii sio ya Taifa mbali imelenga masilshi ya CCM na mafisadi wake, Siku zote Africa viama tawala vina matatizo haishi kwa kujifunza kwa matukio yanayo tokea katika nchi zingine na ulimwengu kwa ujumla wake nadhani CCM wanafikiria kuwa Watanzania wa 1991 ndio wa leo sio kabisa.
    Wanayo yafanya saiz wanajitungia vitanzi na mabom ambayo kwa baadae watashidwa kuyathibiti. hatuombee kufika huko ila tutalazimika ikibidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles