24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein: Elimu bure ililenga kuwakomboa watoto wa masikini

MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alisema hatua ya Serikali kutangaza elimu bila malipo Septemba 23, 1964, ililenga kuwakomboa watoto wa wanyonge.

Alisema kabla ya mapinduzi matukufu ya 1964, watoto wa masikini walikosa kabisa fursa ya kupata elimu, kutokana na kukosa uwezo wa kuigharimia.

Dk Shein aliyasema hayo jana katika hafla ya ufunguzi wa skuli ya msingi na Sekondari ya Bwefum ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea kumbukumbu ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Alisema kabla ya Mapinduzi hayo, zanziabr ilikuwa na skuli chache ambapo watu wenye uwezo pekee ndio waliopata fursa ya kupeleka watoto wao shule.

“Katika ukanda wa maeneo ya Kiembesamaki hadi Bwefum kulikuwa na skuli chache zilizojengwa, ikiwemo  Skuli ya msingi Kombeni iliyojengwa mwaka 1935, Kiembesamaki (1943) na Bwefum mwaka 1956.

“Skuli ya mwanzo ambayo ilitumika zaidi kwa watoto wa Kiafrika ilikuwa ni Dole iliyojengwa mwaka 1935, sambamba na skuli ya Uzini, Wilaya Kati Unguja.”alisema Dk Shein.

Aidha alieleza kuwa  Mapinduzi ya 1964, yameifanya Zanzibar kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya elimu kwani kabla ya Mapinduzi hayo kulikuwa na  skuli zisizozidi 60 tofauti na sasa ambapo zimefikia zaidi ya 400.

Kuhusu elimu ya juu, Dk Shein alisema Zanzibar hivi sasa ina vyuo vikuu vitatu, wakati ambapo miaka 22 iliyopita hakukuwa na chuo kikuu hata kimoja.

Dk. Shein alirudia kauli yake kwa kuwataka wazazi na walezi kutokuchangia mahitaji ya elimu kwa watoto wao kwa vile serikali tayari imefuta michango yote katika skuli za msingi na sekondari.

Aidha, aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kusimamia na kuhoji  mwenendo wa mapato ya Serikali, pale panapotokea kuna shaka.

Alieleza kuwa ukusanyaji bora wa mapato ndio unaoiwezesha serikali kutekeleza malengo yake ya maendeleo, kupitia sekta mbali mbali, kama vile elimu, afya, viwanda na nyenginezo.

Katika hatua nyengine, Dk. Shein alisema Serikali imepunguza kiwango cha kupokea misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo kutoka asilimia 30.2 mwaka  2010 hadi kufikia asilimia 7.2.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles