25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Shein azungumzia miaka tisa ya kuiongoza Zanzibar

Mwandishi wetu-Dar es Salaam

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuridhishwa na mafanikio yaliopatikana Zanzibar chini ya uongozi wake.

Dk. Shein ambaye ni Rais wa awamu ya saba wa visiwa hivyo, aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) Chande Omar Omar, kufuatia kutimiza miaka tisa ya uongozi wake.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Ikulu ya Zanzibar, ilisema Rais Sheid alisema anafurahia miaka tisa ya uongozi wake kutokana na mafanikio yaliopatikana Zanzibar ambayo alisema yametokana na kutekeleza mambo ya msingi ikiwemo ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 na 2015-2020.

Alisema inatakiwa baada ya kumaliza uchaguzi, chama kilichoingia madarakani kinatakiwa kutekeleza ahadi zake jambo ambalo ndilo lililofanywa na Serikali anayoiongoza ambayo imetekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi ilizoahidi ndani ya kipindi cha miaka tisa ya uongozi wake.

 Dk. Shein alisema amefurahi kuona katika uongozi wake mafanikio yamepatikana katika utekelezaji wa Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Zanzibar awamu ya pili (Mkuza II) alioanza nao na Mkuza III unaondelea hivi sasa.

Alisema Serikali anayoiongoza imeendeleza umoja na mshikamano wa wananchi wa Zanzibar kwa kutambua kuwa bila ya kuwepo kwa umoja na mshikamano, hapatakuwa na maendeleo endelevu.

Alisisitiza azma ya CCM ni kutekeleza umoja na mshikamano na ndio maana katika kipindi chote cha uongozi wake wa miaka tisa ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Zanzibar umeimarika.

Alieleza Serikali zote mbili ile ya bara na Zanzibar zinaendelea kusimamia amani na usalama uliopo nchini na kusisitiza kuwa ndani ya miaka tisa, nchi imekuwa salama.

Dk. Shein alieleza sekta nyingi za maendeleo zimeimarika katika kipindi hicho  ambapo Serikali imetekeleza kwa kiasi kikubwa shughuli za kijamii zikiwemo huduma za afya, elimu, suala zima la kuangalia hali za wananchi na shughuli za maendeleo.

Alieleza umhimu wa kuongeza bidii ili uchumi uendelee kukua kwa kasi zaidi ambapo alipoingia madarakani kasi ya ukuaji ilikuwa asilimia 4.3 na sasa ni asilimia 7.1.

Alisema  ukuaji huo umetoa mwelekeo wa kuweza Zanzibar kufikia nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020 huku akieleza dhamira yake kwa kipindi kilichobakia kwamba atafanya jitihada kuhakikisha kasi ya ukuaji uchumi inafikia asilimia 7.5 Juni mwakani.

Alieleza kwa upande wa mfumko wa bei umepungua kwani alikuta ukiwa asilimia 6.1 na hivi sasa umefikia  asilimia 3.9.

Alisema katika kipindi chake juhudi zimechukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, skuli za kisasa katika ngazi zote zikiwemo za maandalizi,  msingi na sekondari.

Alisema skuli 13 za ghorofa zizmejengwa zikiweko tisa kutoka mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na tatu kutoka kwa washirika wa maendeleo na moja iliyojengwa na Said Salim Bakhresa.

Alisema huduma za afya zimeimarika kwa ikilingalishwa na nchi nyingine za bara la Afrika na hata nje ya bara hilo.

Alisema vituo vya afya vina kidhi mahitaji ya wananchi na mgonjwa haendi zaidi ya kilomita tano kupata huduma hizo.

Alisema alipoingia madarakani kulikuwa vituo 135 na hivi sasa kuna vituo 160 Unguja na Pemba.

Kuhusua uimarishaji wa sekta ya utalii, alisema lengo la  Ilani lilikuwa kupokea watalii 500,000 ifikapo mwaka 2020 na tayari limeshafikiwa kabla ya wakati huo na kwamba mwaka jana Zanzibar ilipokea watalii 520,809.

Alisema hivi sasa kumekuwa na ongezeko la mashirika ya kigeni kuleta wageni Zanzibar kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Urusi, Ulaya Mashariki jambo linaloleta matumaini kwamba Zanzibar inaweza kupokea watalii 700,000 ifikapo mwaka 2020.

Alieleza kuwepo pia afya bure, elimu bure na kuwepo kwa miasingi ya utawala bora na haki za binaadamu, uhuru wa kuabudu na uvumilivu wa dini hapa Zanzibar.

Hata hivyo, alieleza changamoto zilizopo ikiwemo suala zima la ajira ambapo tayari Serikali imeweka miakati ikiwa ni pamoja na kuweka mifuko maalum ukiwemo wa kuwaewezesha kiuchumi wajasiriamali na wa  vijana.

 ambapo kwa upande ule wa vijana  tayari bilioni 46 zimetengwa.

Alisema kwa sasa utegemezi wa bajeti ya Zanzibar  umepungua kutoka asilimia 30.2 mwaka 2010 hadi asilimai 6 sasa hali ambayo imechangiwa na juhudi zilizochukuliwa katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Alisema Serikali yake kwa mwezi inakusanya Sh bilioni 67 ambapo mwaka 2010 ilikuwa ikikisanywa Sh bilioni 13.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles