24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Dk. Shein awataka wafanyabiashara kutotumia corona fursa kupandisha bei za bidhaa

Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed shein amewataka wafanyabiashara wote visiwani humo kuendesha biashara zao kwa uadilifu na wasitumie sababu ya kuwepo kwa janga la maradhi ya corona kuuza bidhaa kwa bei kubwa hasa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Dk. Shein amesema hayo leo Alhamisi Aprili 23, katika hotuba ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kila mwaka ukikaribia mwezi huo mtukufu.

“Nawapongeza wafanyabiashara kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha bidhaa zote muhimu hasa za chakula zinapatikana kama kawaida tangu yalipoingia maradhi hayo ni matumaini yangu kwamba hali hiyo itaendelea katika mwezi wa Ramadhani na miezi mingine inayokuja.

“Aidha, nitoe wito kwa ndugu zangu waumini wa dini ya Kiislamu kumkumbuka sana Mwenyezi Mungu na kumtukuza pamoja na kusoma dua mbalimbali katika funga na sala zao za faradhi na sunna katika mwezi wa Ramadhani na miezi mingine ili tuzidi kupata rehema na ulinzi wake,” amesema Dk. Shein.

pamoja na mambo mengine, akizungumzia ugonjwa wa corona Dk. Shein amesisitiza kuwa miongoni mwa mambo muhimu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo ni kujiepusha na mikusanyiko ya watu ingawa suala hilo limekuwa changamoto kubwa lakini ni lazima litekelezwe kwa sababu mikusanyiko ndio njia mojawapo inayosababisha maambukizi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles