23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

DK. SHEIN AWAONYA WASAKA URAIS ZANZIBAR

Is-haka Omar, Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewaonya baadhi ya watu wanaofanya kampeni za kusaka urais wa Zanzibar kabla ya muda wa kufanya hivyo kufika na kusisitiza kuwa yeye bado ni Rais wa Zanzibar.

Amesema kuna baadhi ya viongozi wa chama na serikali tayari wameanza kupanga timu za urais badala ya kushughulika na mambo ya msingi ya kufanya shughuli za chama zitakazofanikisha kuiweka serikali madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.

Dk. Shein ametoa onyo hilo leo katika ziara yake ya kutembelea mashina ya chama hicho katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

“Nafasi ya urais ndani ya CCM haipatikani kwa kampeni na makundi yasiyo halali bali kwa utaratibu maalumu kupitia vikao vya kikatiba ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba na miongozo na kanuni  mbali mbali za CCM,” amesema.

Dk. Shein pia amebainisha kuwa watu hao wasipoacha tabia hiyo na kuvumilia hadi 2020, atawachukulia hatua kali za kinidhamu zikiwemo kufikishwa katika vikao vya usalama na maadili vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ili wahojiwe na kuchunguzwa dhidi ya mwenendo wao  juu ya mwenendo wao usiokuwa na manufaa kwa CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles