31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

DK. SHEIN AWAFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA PEMBA

NA SULEIMAN OMAR-PEMBA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amewatembelea na kuwapa pole wananchi wa maeneo mbalimbali kisiwani Pemba kutokana na maafa yaliyowapata, yaliyotokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

Mvua hizo zimeathiri baadhi ya makazi ya wananchi, mazao na miundomninu ya barabara na madaraja kisiwani humo.

Akizungumza katika ziara yake hiyo, alielezea kusikitishwa na hali hiyo huku akitoa pongezi kwa wananchi ambao wameshikamana na kusaidiana bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Maeneo aliyoyatembelea ni Mchanga wa Kwale, Chamanangwe, Bugujiko, Kuungoni, Gando na Pujini kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na barabara ya Mgagadu Kiwani, Chonga, Changaweni Mkoani, ghala la karafuu la ZSTC Mkoani na Makombeni kwa upande wa Mkoa wa Kusini Pemba.

 Dk. Shein aliwaeleza wananchi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko pamoja nao na itaendelea kuwapa kila msaada unaohitajika, huku akiwataka kuwa na uvumilivu na subira na kutomlaumu mtu.

“Hakuna dhiki wa dhiki bali baada ya dhiki ni faraja… basi wananchi endeleeni na subira,” alisisitiza Dk. Shein.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles