Dk. Shein asisitiza wajibu wa wadhamini

0
335

MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa maofisa wadhamini wanadhima kubwa ya kuwasimamia wale wote wanaovunja misingi ya kukuza uchumi hapa nchini.

Dk. Shein aliyasema hayo jana katika Kiwanda cha Mafuta na Makonyo Wawi wakati alipokutana na watendaji na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na viongozi wa vikosi vya SMZ na SMT wanaofanya kazi zao kisiwani Pemba.

Rais Dk. Shein alisema kuwa kwa mwaka jana kasi ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar ilifikia asilimia 7.1 na matarajio ni kukua kwa uchumi huo mwaka hadi mwaka kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Alisema kuwa mapato yanakusanywa kwa ufanisi mzuri na kinachokusanywa ndicho kinachotumika na hakuna tatizo la matumizi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hivi sasa.

Alisema kuwa kuhusiana na mapato Rais Dk. Shein alisema kuwa wakati anaigia madarakani mwaka 2010 Serikali ilikuwa ikikusanya Sh bilioni 13.5 kwa mwezi ambapo kwa hivi sasa Zanzibar inakusanya Sh bilioni 65.7 kwa mwezi.

“Mambo mengi yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yanatekelezwa kutokana na fedha zake wenyewe ambapo licha ya kukusanywa kiasi hicho cha fedha lakini bado hakitoshi, hivyo juhudi zaidi zinahitajika,” alisema

Rais huyo wa Zanzibar, alisema kuwa mbali ya juhudi hizo za Seriakli lakini bado wapo wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na kusisitiza kuwa Serikali zote duniani zinakwenda kwa kukusanywa kodi.

Alitumia fursa hiyo kusisitiza haja ya kulipa kodi sambamba na kutoa risiti kwani bila ya kutoa ama kuchukua risiti mapato makubwa ya Serikali yanapotea.

Kuhusiana na suala la mfumko wa bei, Rais Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar uko chini ambapo wakati anaingia madarakani ulikuwa asilimi 18 na kila siku unashuka na hadi hivi leo uko chini ya tarakimu moja huku bei ya bidhaa hivi sasa imepungua sana.

“Licha ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bidhaa bei pamoja na kufanya magendo lakini hata hivyo, juhudi zinaendelea kuchukuliwa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanaishi vizuri.

“Kuna kila sababu ya wananchi wa Zanzibar kutibiwa bure sambamba na kupewa huduma zote za uchunguzi wa afya na kuitaka Wizara ya Afya kusimamia kwa wale wote watakaofanya hadaa washtakiwe kwa kuhujumu uchumi,” alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here