25.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

DK .SHEIN AMEWAKOMESHA WALAFI MAFUTA, GESI – UVCCM

Na Mwandishi Wetu-Zanzibar

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM ) imepongeza msimamo uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuhusu umakini wa mikataba ya uchimbaji wa mafuta na gesi asilia visiwani humo.

Imesema hiyo ndiyo njia pekee muhimu na bora kuliko zote inatakayoleta manufaa na kutetea maslahi ya jamii ikiwa mikataba yote tangu sasa itasimamiwa kwa weledi, umakini na uzalendo.

Akitoa tamko la umoja huo   mjini Unguja jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM,  Shaka Hamadu Shaka, alisema nchi za Afrika zimerudi nyuma kwenye uchumi  huku watu wake wakiendelea kubaki katika lindi la umaskini.

“Nchi za Afrika Mungu ameziruzuku raslimali na maliasili, hizo ni nyenzo za kujijenga kwenye uchumi na kupiga hatua ya maendeleo.

“Mnapozubaa katika utiaiji saini mikatata, mnajikwamisha nyinyi wenyewe, matokeo yake tija  hubaki mikononi mwa watu wachache bila kuwanufaisha wananchi katika kupambana na umasikini,” alisema Shaka.

Alisema ikiwa  utakuwapo  umakini na uzalendo nchi ndogo kama Zanzibar ni rahisi kupiga hatua na kujijenga katika uchumi pamoja na watu wake wakanufaika na  maisha.

“Hotuba ya Rais Dk. Shein katika Baraza la Idd  ilikuwa ya uzalendo ilitazama mbele katika siku nyingi zijazo na manufaa yake, amewaasa na kuwataka watendaji kujali nchi kwanza.

“Haya ndiyo mambo yanaoyohitajiwa na wananchi, utaifa mbele na ubinafsi usipate nafasi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles