24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein akaribisha wawekezaji

Dk. Ali Mohamed Shein
Dk. Ali Mohamed Shein

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Zanzibar iko tayari kushirikiana na wawekezaji ili kusaidia kuinua uchumi wake na kuimarisha ustawi wa wananchi wake.

Akizungumza Ikulu jana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania Cooperation Limited, Bruce Zhang, Dk. Shein alisema wawekezaji wanakaribishwa Zanzibar kuwekeza katika sekta zote za uchumi na kijamii.

“Wawekezaji wakiwamo Kampuni ya Huawei wanayo fursa ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika sekta zote ikiwamo nishati, teknolojia ya habari na mawasiliano, viwanda, uvuvi na kadhalika.

“Miradi ya pamoja tunaikaribisha na tuko tayari kushirikiana na kampuni ya uwekezaji kuendesha miradi ya pamoja hivyo milango iko wazi,” alisema Dk. Shein.

Dk. Shein alimweleza Zhang kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianzisha Programu ya Miji Salama miaka miwili na nusu iliopita na utekelezaji wake unaendelea vema, hivyo kujitokeza kwa Huawei kuunga mkono progamu hiyo, ni habari njema kwa Serikali na wananchi wa Zanzibar.

Awali Mkurungenzi Mtendaji wa Huawei alimueleza Rais Shein kuwa kampuni yake inatarajia kupanua shughuli zake kwa kuongeza huduma na kusaidia sekta ya elimu, afya na kuendeleza dhana ya miji salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles