28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein aeleza sababu za nchi kuwa madhubuti

MWANDISH WETU-PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema umadhubuti wa nchi pamoja na utajiri wake unategemea kwa kiasi kikubwa jinsi gani ilivyojidhatiti katika kuendeleza na kudumisha utawala wa sheria (Utawala Bora).

Dk. Shein aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliyofanyika   katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Wete Pemba, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema   maadhimisho ya Siku ya Sheria yana umuhimu mkubwa katika kutoa mwamko kwa wananchi katika kuzifahamu na kuzitii sheria za nchi zikiwa ndiyo msingi mkubwa wa kukuza utulivu, amani na maendeleo.

Aliongeza kuwa suala la kuzifahamu na kuzitii sheria husababisha  kuishi kwa nidhamu na misingi ya kuheshimiana katika maisha ya kila siku kwa sababu sheria lazima zitambuliwe  wananchi waweze kupambanua haki na wajibu.

Dk. Shein alisema  ikiwa jamii itaishi bila ya kuzifuata sheria basi utakosekana ustaarabu katika utekelezaji wa mambo kwa sababu  sheria ni suala nyeti linalogusa maisha katika nyanja mbalimbali.

  Rais Dk. Shein pia aliwahimiza wananchi wote kuendelea kutii sheria za nchi kama Katiba inavyoelekeza huku akiwahiziwa viongozi wa dini zote zinazofuatwa na wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla kuendelea kuhubiri utii wa sheria za nchi.

Alieleza kufurahishwa na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo; “Uimarishaji wa Taasisi za Umma ni Ustawi Bora wa Upatikanaji wa Haki kwa Jamii”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles