23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Sengati: Mtoto hana mbadala, alindwe kwa ustawi wa Taifa

Na Anthony Ishengoma- Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati amewataka wazazi na walezi pamoja na vyombo vya usalama Mkoani Shinyanga kuchukia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kwa kuwa hakuna mbadala watoto katika ustawi jamii kokote duniani.

Dk. Sengati amesema hayo jana Juni 16, 2021 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika Kata ya Chibe nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga na kuwataka wadau wa masuala ya  watoto pamoja na wazazi mkoani Shinyanga kuchukia ukiukwaji wa haki za watoto kwa ustawi wa jamii ya Tanzania.

‘’Nitakuwa mkali sana kwa wale wananchi wasio kuwa na maadili mamema, wasio kuwa na nidhamu, wasiokuwa wazalendo na wanaocheza cheza na haki za watoto ni lazima kuhakikisha watoto wanasoma, wanalindwa na wanakula vizuri ili kulinda haki zao,’’ aliongeza Dk. Sengati.

Aidha, Dk. Sengati alisema kuwa ni lazima jamii ikubali watoto wanapewa haki ya kujieleza na kushirikishwa katika masuala yote yanayohusu ustawi wao katika Taifa la Tanzania ndio maana Umoja wa Afrika ukatenga siku hii muhimu kuadhimisha Siku ya mtoto wa Afrika na lazima na Tanzania sio kisiwa hivyo kuna ulazima kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Yasinta Mboneko amesema amekuwa mstari wa mbele kutembelea shule mbalimbali katika Wilaya yake ili kuhakikisha watoto wanalipiwa ada lakini pia kujionea kama watoto kweli wanaenda Shule ili kuweza kutimiza ndoto zao.

Aidha, Mboneko alionesha kutambua mchango wa Taasisi za dini kwa mchango wao wa malezi na elimu kwa watoto na kuonya wale wote watakao shiriki katika kuminya haki za watoto kupata elimu atahakikisha wanashughulikiwa uku akiwaomba walezi hususani akina mama kuendelea kuwasimamia watoto ili wasije wakaangukia katika mikono isiyo salama.

Wakati huo Mkurugenzi wa Shirika la African Youth Festival Shinyanga, Justa Denis amesema Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mtoto ni vitu viwili vinavyokinzana kwani zinatoa fursa kwa wazazi wasioelimika kukatili watoto lakini pia kukatiza ndoto za mtoto wa kike kufikia ndoto zake na kwa maoni yake haoni kama kuondolewa kwa sheria hizo kutaongeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Young Women Leadership Shinyanga, Beatrice John ameiomba serikali kufikirai upya suala la watoto wanaopata ujauzito wakiwa shule kurudi tena darasani kwa kuwa baadhi yao wanapata ujauzito kwa kubakwa na kushawishiwa na hivyo kurudi kwao shule kutawasaidia wao kutoa msaada mkubwa katika kuendeleza familia yao.

Aidha, Beatrice John ameongeza kuwa wapo watoto wakiume ambao wanakosa fursa ya kusoma kutokana na kuajiliwa wakiwa wadogo na hivyo kukosa fursa pia ya kufikia ndoto zao na hivyo kuitaka serikali kuzidisha nguvu katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Mkoa wa Shinyanga imeungana na mikoa mingine Nchini kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hudhimishwa kila ifikapo Juni 16 baada ya mauaji ya Kimbali yaliyotokea Soweto Afrika ya kusini na kupelekea watoto wengi kupoteza maisha na kupelekea Umoja wa Afrika kutenga Siku hii muhimu kuwa Siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles