22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Samia anastahili pongezi kwa kuimarisha Diplomasia, Uchumi Tanzania na China

Na Mwandishi Wetu Mtanzania Digital

Tunapoelekea kufunga mwaka 2022, ubalozi unatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa Majukumu ya Ubalozi.

Katika Mwaka 2022 mambo mbalimbali yenye tija na manufaa kwa wananchi yamefanyika kufuatia mwongozo na maelekezo ya Mwanadiplomasia No 1 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyofanyika

MOJA 

Tarehe 2-4 Novemba 2022 Ilifanyika Ziara ya Kihistoria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk. Samia Suluhu Hassan-nchini China. Kupitia ziara hiyo Tanzania na China zilipandisha hali ya mahusiano kuwa ya Kimkakati katika nyanja zote.

MBILI
Kwa upande wa biashara, Mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la China yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani Milioni 409 hadi kufikia Dola za Kimarekani Milioni 605.5. Inatarajiwa katika mwaka 2023 mauzo yataongezeka kwa asilimia 20 kutokana na Tanzania kufunguliwa soko jipya la bidhaa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan nchini China;

TATU
Wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshughulika na zao la Parachichi walifunguliwa soko jipya la China Mwezi Novemba 2022. Kuanzia msimo ujao wa 2023 mauzo ya parachichi katika soko la China yataanza.

NNE
Wavuvi wa Tanzania walifunguliwa soko Jipya la kuuza mabondo ya Samaki na samaki aina sangara nchini China Mwezi Novemba 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 mauzo ya bidhaa za uvuvi yataongezeka.

TANO
Bidhaa za Tanzania zilizoongezewa thamani zilianza kuuzwa katika soko la China kupitia Mtandao Maarufu wa Biashara wa JD.COM wenye watumiaji milioni 600- Mei 2022.

SITA
Watanzania walianza kufanya shughuli za usafirishaji wa mizigo yao moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China kwa kutumia Shirika la Ndege la Air Tanzania- Mei 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 baada ya China kufunguka shughuli zitaongezeka.

SABA
Usafiri wa abiria wa ndege wa moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou ulianza Mwezi Julai 2022. Kuanzia Mwezi Januari 2023 Wafanyabiashara,wanafunzi & watalii watanufaika na huduma hiyo baada ya hatua ya China kufungua mipaka na kuondoa masharti ya udhibiti wa UVIKO-19

NANE
Kufuatia maelekezo ya Mhe Rais Dk. SuluhuSamia Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika jijini la Biashara la China- Guangzhou ulifunguliwa rasmi mwezi Mei 2022. Watanzania wameanza kupata huduma mbalimbali za kufanikisha shughuli zao za biashara na Ubalozi mdogo umeanza kufungua fursa mpya za masoko ya bidhaa.

TISA
Filamu ya Tanzania Royal Tour ilioneshwa katika Televisheni ya Hainan Mwezi Oktoba 2022 na kutizamwa na watu milioni 60. Aidha filamu hiyo iliyotafsiriwa kwa lugha ya kichina imeoneshwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ya China ikiwemo Bilibili m.bilibili.com/video/BV1jB4y1…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles