Dk.Ndumbaro: Sio rahisi kuridhia mikataba yote

0
1055
Naibu Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro

Anna Potinus

Naibu Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro amesema sio mikataba yote ambayo imesainiwa na serikali inaweza kuridhiwa kutkana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi kukinzana na mila na desturi za nchi.

Dk. Ndumbaro ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 13, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi aliyetaka kujua idadi ya mikataba iliyosainiwa na nchi lakini haijaridhiwa .

“Ni mikataba mingapi ya kimataifa ambayo nchi imesaini lakiNi haijaridhiwa na je kuna adhari zozote kwa nchi kutoridhia mikataba ambayo tayari imeshaisaini,” amehiji.

Akijibu hoja hiyo Dk.Ndumbaro amesema mikataba sio rahisi kuridhia mikataba yote inayosainiwa kutokana na baadhi kukinzana na imani za dini, mila na desturi pamoja na sheria za nchi.

“Katika bunge hili linaloendelea tuna mikataba takribani mitatu ambayo imeletwa kwaajili ya kuridhia lakini sio yote ambayo inaweza kuridhiwa kwasababu mingine inakinzana na mila na desturi zetu, imani za dini, sheria ambazo tumezitunga, katiba pamoja na mambo mengine ambayo hatuwezi kuyaelezea,” amesema Dk.Ndumbaro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here