23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Ndumbaro atengua zuio la Kigwangalla Green Mile

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro ameirejeshea kitalu cha uwindaji cha Lake Natron Game Contolled Area-East  Kampuni ya Green mile safaris limited hadi mwaka 2022.

Hatua hiyo imekuja kufuatia, awali aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo,Dk.Hamisi Kigwangalla kwa kutumia mamlaka yake chini ya Kifungu cha 38 cha Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Sura ya 283 alimfutia Muomba Mapitio umiliki wa kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area – East kwa barua yake yenye Kumb. Na. CBA.177/389/01/281.

Kutokana na hali hiyo Kampuni hiyo ilimwandikia Waziri barua yenye Kumb. Na. GMS/0571.19.002.Let2, ya Agosti  9 mwaka 2019 ikionesha kutokubaliana na uamuzi wa Mheshimiwa Waziri na ikiomba  mapitio ya uamuzi huo.

Maombi hayo ya Mapitio ya Kiutawala yalifanyika kwa mujibu wa kifungu cha 38 (14) cha Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, ambacho kinamtaka mtu yeyote asiyeridhika na uamuzi wa Mheshimiwa Waziri wa kufuta umiliki kitalu cha uwindaji kuomba marejeo ya kiutawala kwa Mheshimiwa Waziri husika.

Hali hiyo ilimlazimu Waziri wa sasa wa Wizara hiyo Dk.Damas Ndumbaro kwenda katika kitalu husika katika eneo la Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya kujionea hali halisi.

Akitangaza uamuzi huo leo,Alhamisi Aprili 29 mwaka huu  Jijini hapa,Waziri Ndumbaro amesema Muomba Mapitio hakupewa nafasi ya kusikilizwa kama kifungu cha 38(13) cha Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009 kinavyoelekeza hivyo maamuzi ya Waziri yamekwenda kinyume na misingi ya haki za asili. (principles of natural justice).

Pia amesema Muomba Mapitio amefanya uwekezaji wa ujenzi mkubwa katika kitalu husika kwa kujenga loji na Kambi ya malazi ya Nyota Tano na kujenga miundombinu ya Maji, Barabara na Umeme katika eneo la kitalu.

“Muomba Mapitio amefutiwa umiliki wa kitalu katikati ya msimu wa uwindaji wa kitalii na tayari alikuwa na miadi na wageni hadi Desemba 31, 2019. Aidha, wakati huo baadhi ya wageni walikuwa katikati ya safari za kuwinda hivyo kufuta umiliki wa kitalu si kwamba umeleta hasara na usumbufu kwa wageni bali hasara kwa Serikali,”amesema

Pia amesema Kufuta umiliki katikati ya msimu wa uwindaji unaharibu sifa ya Tanzania kama mahali salama pa kufanya uwindaji na inazorotesha juhudi za serikali za kuendeleza utalii.

Kutokana na hali hiyo,Waziri huyo wa Maliasili na Utalii ameagiza Kampuni hiyo irejeshewe  umiliki wa kitalu hicho hadi mwaka  2022.

“Iandaliwe rasimu “template” itakayotumiwa katika umilikishaji wa vitalu itakayoonesha “terms and conditions” za kufuatwa na mwekezaji wakati wote wa umiliki wa kitalu,Kuwepo kwa umakini wakati wa kuandika nyaraka za kiofisi, ili kuepusha ukinzani wa sheria na taratibu zilizopo,”amesema.

Pia amesema kuweka utaratibu wa kushughulikia migogoro haraka pindi inapojitokeza.

“Haki ya mwekezaji inaisha pale ukomo wa umiliki unapofika kwa mujibu wa kipindi cha umiliki kilichopo ki-sheria bila kujali kiwango cha uwekezaji alichofanya.Kama kuna mtu yoyote ana malalamiko ayalete kwa Mheshimiwa Waziri kimaandishi na sio kuleta fujo na taharuki katika jamii,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles