24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Ndumbaro apongeza ‘Ngorongoro Live Streaming’ maonyesho ya Dubai Exp2020

Na Mwandoishi Wetu, Dubai

Waziri wa Maliasili na Utallii, Dk. Damas Ndumbaro amepongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa namna inavyotangaza vivutio vya Utalii kwa njia kidigitali kupitia Ngorongoro Live  Streaming(Matangazo mubashara kutoka Ngorongoro).

Amesema hali hiyo ya Ngorongoro Streaming Live kwenye maonesho hayo ya Exp2020 Dubai, inakomesha upotoshaji uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watu wa nchi jirani juu ya vivutio vizuri vya Utalii vilivyopo Tanzania na kusema kuwa vipo nchini mwao.

 “Tayari kama nchi tumekuja na njia ya kutangaza vivutio vya utalii kwa njia ya Kiditaji kupitia: NgoroNgoro Live  Streaming”na meanza kuonesha matunda ya wazi katika Maonesho haya.

Aidha, Dk.Ndumbaro amebainisha kuwa: “Tumekuwa tukirusha matukio mbashara kutoka katika Eneo la Hifadhi ya NgoroNgoro, hii imelifanya banda la Tanzania kuwavutia maelfu ya watu kuja kujionea maajabu yaliyopo Tanzania.

“Tunachotaka kwa sasa ni kuhakikisha Maonesho makubwa ya Kibiashara Tanzania inashiriki kikamilifu huku msisitizo mkubwa kama nchi ni kunadi utajiri wa vivutio vya utalii tulivyonavyo ili kuuondoa ule upotoshwahi wa majirani zetu,” amesema Dk. Ndumbaro.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndumbaro ametoa wito kwa Watanzania popote walipo kutumia fursa ya kunadi vivutio vya utalii walivyonavyo kwani kufanya hivyo ni ishara  uzalendo kwa nchi yao.

Miongoni mwa taasisi za Tanzania za Wizara ya Maliasili na Utalii  zinazoshiriki maonesho hayo ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyanapori Tanzania (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Huduma za Misitu Tazania (TFS).

Maonesho hayo ya kimataifa yaliyoanza  Oktoba Mosi mwaka 2021 yanaendelea hadi Machi 31, mwaka huu na yanashirikisha zaidi ya nchi 192.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles