23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MWELE MALECELA APATA KAZI UN

Na MWANDISHI WETU-DAR E SALAAM


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Mwele Malecela amepata kazi Shirika la Afya Duniani kwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Afrika wa Umoja wa Mataifa (WHO-AfRO).

Dk. Mwele ambaye  ni mwanamke wa kwanza kuongoza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), uteuzi wake ulitenguliwa Desemba 17, mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli baada ya kutoa taarifa za kitafiti kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika.

Taarifa za uteuzi wake huo zilianza kusambaa jana asubuhi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ambapo ilieleza kuwa mtaalamu huyo wa magonjwa ya binadamu aliondoka nchini na kwenda katika kituo chake kipya cha kazi nchini Congo Brazaville.

Baada ya uteuzi wake huo, Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya SIKIKA,  Irenei Kiria, alimpongeza kupitia mtandao wa kijamii wa tweet kwa kuandika kuwa.

“Kila la heri rafiki yangu Mwele Malecela katika nafasi yako mpya ndani ya WHO katuwakilishe,” alisema.

Naye Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, alipongeza mtaalamu huyo wa magonjwa ya binadamu kwa kupata kazi hiyo kubwa ya kimataifa.

“Kwa dhati nampongeza kwa nafasi yake hiyo mpya…hii imeonyesha ni namna gani alikuwa mtu muhimu hapa nyumbani japokuwa msimamo wake wa kitaaluma ulimgharimu pale aliposimamia tafiti.

“Ni funzo kwa serikali zetu kukubali kupokea mambo hata kama hawapendi kusikia ni vema zikawa zinaheshimu taaluma na kuachana na siasa wakati mwingine.

“Narudia tena kumpongeza dada yangu kwa nafasi hiyo muhimu ambayo pia itailetea taifa sifa nje na ndani ya Bara la Afrika ,’’aliongeza Kilewo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles