25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa awapa maelekezo watumishi wa afya

ELIUD NGONDO-MBEYA

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi, Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka watumishi wa umma kuzingatia sheria na maadili ya kazi zao wanapowahudumia wananchi ili kuepuka migogoro.

Dk. Mwanjelwa alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na watumishi wa Kituo cha Afya Iyunga cha jijini Mbeya.

Pia, Dk. Mwanjelwa alikuwa akitoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwenye kituo hicho pamoja na vituo vingine vya afya na katika shule za msingi.

Dk. Mwanjelwa ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Mbeya kupitia CCM, aliwataka wahudumu wa afya katika vituo hivyo vya afya, zahanati na kwenye hospitali, wawahudumie wagonjwa kwa upendo ili kuokoa maisha yao kwa kuwa kazi yao ni wito.

“Nawaomba wafanyakazi wa sekta ya afya, kuweni na moyo wa huruma kwa wagonjwa wetu kwani Serikali inatambua changamoto mbalimbali mnazokumbana nazo pindi mnapotoa huduma.

“Pamoja na hayo, jitahidini kuvumilia na kutoa huduma kwa moyo ili kuokoa maisha ya watu,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Mbali na Kituo cha Afya cha Iyunga, pia alitoa msaada wa vifaa katika Kituo cha Afya Nzovwe na baadhi ya shule za sekondari na msingi za jijini Mbeya ili kupunguza changamoto zinazowakabili maeneo hayo.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, James Kasusura, alimshukuru Naibu Waziri huyo na kusema msaada huo utatumika kama ulivyokusudiwa ili kuboresha miundombinu ya afya na elimu.

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi, alimwomba Dk. Mwanjelwa asichoke kuendelea kuchangia maendeleo kwani uhitaji wa vifaa mbalimbali vya afya na shule bado ni mkubwa katika Jiji la Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles