25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa ataka ubunifu kwa watumishi

MWANDISHI WETU-MOROGORO

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka waajiri serikalini kuzingatia kigezo cha ubunifu wanapotekeleza hatua ya  ujumuishwaji wa masuala ya  jinsia sehemu za kazi ili kuleta matokeo chanya na yenye tija katika kutekeleza  majukumu yao ya kila siku.

Hayo aliyasema jana mjini Morogoro, alipofungua kikao kazi cha siku mbili kinachohusu ujumuishwaji wa masuala ya  jinsia mahali pa kazi.

Alisema endapo waajiri watazingatia kigezo cha ubunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea serikali itapata watendaji kazi bora watakaoleta matokeo chanya katika maendeleo ya nchi kwa vile watafanya kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi.

“Tunapodai haki zetu kama wanawake tuwe na hoja zenye mashiko zitakazoendana na sifa na vigezo husika, tusiseme kuwa sisi ni wanawake hivyo tupewe nafasi,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Aliwataka waajiri kuzingatia vigezo vya ubunifu wanapoajiri wanawake na kutenga bajeti kwa ajili ya ujumuishwaji wa masuala ya jinsia mahali pa kazi  kuboresha  utendaji kazi.

  Mwanjelwa aliwaagiza watendaji katika Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuwa kioo katika utekelezaji wa masuala ya jinsia mahali pa kazi  kuepuka vitendo vya unyanyasaji wa jinsia, rushwa ya ngono, ubaguzi wa aina yoyote, upendeleo, ubadhirifu wa mali za umma na uvujishaji wa siri za serikali.

  Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Agnes Meena, alisema ofisi yake kama mratibu wa masuala ya anuai za jamii imeona umuhimu wa kuandaa kikao cha ujumuishaji wa masuala ya  jinsia sehemu za kazi kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu kwa kuwa wao ndiyo wahusika katika usimamizi wa mipango ya rasilimali watu na masuala yote ya  utumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles