24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa ataka mafunzo bora kwa watumishi

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kutoa mafunzo bora yenye kuzingatia weledi.

Alisema mafunzo hayo yawajengee uwezo wa  utendaji watumishi wa umma wanaopata fursa ya kujiendeleza katika chuo hicho.

Wito huo aliutoa   Dar es Salaam jana alipozungumza na watumishi wa TPSC makao makuu na Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa ziara yake  yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya TPSC na kujiridhisha na utendaji kazi wa chuo hicho.

Dk. Mwanjelwa aliwahimiza watumishi wa TPSC kuwa wabunifu kwa kuboresha mitaala itakayowaandaa vema watumishi wa umma, sekta binafsi na wananchi wanaohitimu katika chuo hicho  waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa.

Alisema katika dunia ya sasa, jamii inabadilika, uchumi unabadilika na siasa inabadilika pia, hivyo amewataka watumishi wa TPSC wabadilike kwa utendaji wao uwe wenye kujali matokeo na wenye tija.

  Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dk. Henry Mambo, alisema TPSC ilianzishwa  kusaidia hatua ya kujenga uwezo wa watumishi wa umma uwe wenye kujali matokeo katika kutoa huduma bora kwa umma.

Alisema kwa sasa chuo kina matawi sita yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara, Singida Tabora,Tanga na Mbeya.

Alisema madhumuni ya kuanzisha chuo ilikuwa ni kuziba pengo lililokuwapo la kukosekana   chuo rasmi kinachoshughulikia mafunzo ya watumishi wa umma  waendane na mabadiliko yaliyoletwa na maboresho katika utumishi wa umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles