24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwaka aweka wazi huduma zake

Dk. MwakaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MIEZI michache baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamis Kigwangalla, kufanya ziara katika kituo cha cha tiba mbadala cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Dar es Salaam, mengi yamebainika.

Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa Dk. Kigwangwalla    aligundua  tabibu huyo wa tiba mbadala hakuwa na vyeti lakini taarifa zilizopo zinaonyesha Dk. Mwaka na wasaidizi wake walipewa vyeti kwa mujibu wa sheria na Baraza la Tiba Asilia.

Inaelezwa kuwa  Dk. Mwaka amekwisha kukabidhi vyeti hivyo kwa Serikali na MTANZANIA ina nakala zake ikiwa ni kutekeleza agizo alilopewa Desemba 16 mwaka jana na   Naibu Waziri Dk. Kigwangwalla.

Dk. Kigwangwalla amekwisha  kukiri kuwa  vyeti hivyo vimekwisha kufikishwa wizarani  na kuhakikiwa.

Kwa sababu hiyo,  Mwenyekiti  wa Shirikisho la Shirikisho la vyama vya Tiba Asili amesema     hatua hiyo ya Dk. Kigwangwalla haikuwa sahihi  bali ilisababisha  malumbano kwa jamii jambo ambalo si sahihi.

“Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaa na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi ndiyo hasa walikwazika na agizo hilo la wizara.

“Hatimaye Desemba 31 mwaka jana tulifanya kikao cha pamoja kati ya wadau hao, shirikisho na Wizara ya Afya tukiongozwa na uenyekiti wa Waziri Ummy Mwalimu na kukubaliana   baadhi ya mambo lakini si kupiga marufuku matangazo ya tiba mbadala,” alisema Lutenga.

MTANZANIA ilifika katika kituo hicho  kilichopo Ilala Bungoni na kukuta huduma ikiendelea kama kawaida jana.

Hata hivyo,   Dk. Mwaka alisema hataki kuingia katika malumbano na Serikali na  kwa sasa  anasukumwa na utoaji huduma kwa jamii kama sheria inavyotaka.

Alisema kutokana na hali hiyo kituo chake kimeandaa utaratibu maalumu wa utoaji matibabu kwa wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Alisema pamoja na misukosuko aliyoipata, Foreplan Clinic pia imejikita kusaidia jamii kama vile ujenzi wa nyumba za ibada ikiwamo misikiti na makanisa na hata kujihusisha masuala ya michezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles