25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Msonde asisitiza ushirikiano walimu, wazazi

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk. Charles Msonde, amehimiza ushirikiano baina ya wazazi, walimu na wanafunzi ili kuinua zaidi maendeleo ya taaluma na maadili shuleni.

Hayo aliyasema Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Ihsan iliyopo Kigamboni.

Dk. Msonde alisema ushirikiano wa karibu baina ya pande zote utaongeza zaidi ufaulu shuleni na kuinua taaluma.

“Nimezunguka katika shule nyingi, lakini sikuwahi kuona kitu kinachoitwa umoja wa wazazi, walimu na wanafunzi, nawapongeza sana Ihsan Sekondari kwa kuanzisha mfumo huu ambao utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza elimu, maadili na uzalendo kwa taifa,” alisema Dk. Msonde.

Alishauri shule zingine kuanzisha mfumo kama huo kwani unaleta muunganiko mzuri na kuwajenga vijana katika mshikamano, upendo na uzalendo.

“Umoja kama huu unafaa sana kuwepo katika shule zetu kwani licha ya kuongeza mshikamano baina ya walimu, wazazi na wanafunzi, pia huongeza uthubutu kwa wanafunzi na kujikuta wanafanya mambo makubwa zaidi na yenye faida kwa taifa,” alisema Dk. Msonde.

Mkuu wa shule hiyo, Dk. Hashimu Saiboko alieleza kuhusu maendeleo ya shule hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 hadi wanafanikiwa kufanya mahafali ya kwanza ya kidato cha nne.

“Shule yetu imepitia changamoto nyingi tangu kuanzishwa kwake mpaka leo, lakini tunawashukuru wazazi kwa namna walivyoshirikiana nasi katika kuzitatua changamoto hizo na hatimaye tunafanya mahafali haya ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shule,” alisema Dk. Saiboko.

Alitaja idadi ya wahitimu ilikuwa 56 na kati ya hao wavulana walikuwa 30 na wasichana 26 na kusema kuwa vijana hao waliandaliwa vizuri na matumaini yake watafanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles