30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Dk Mpango: Serikali itaendelea kuboresha ukusanyaji takwimu

Na Mwandishi wetu, Kigoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na mifumo ya ukusanyaji wa takwimu ili kuwa na takwimu bora kwa ajili ya kutunga sera na kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuifanyia tathmini na ufuatiliaji mipango hiyo.

Dk. Mpango aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Kigoma.

“Jengo hili litakapokamilika litaboresha utendaji kazi kwa watumishi na upatikanaji na usambazaji wa takwimu kwa wadau wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na hususani wakati huu wa maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwaka 2022” alisema Dk. Mpango

Aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa namna ambavyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi na kuipatia nchi takwimu bora  ambazo ndizo zinatumika katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

 “Mafanikio ya Serikali yetu ya awamu ya tano ambayo tunajivunia yamejengwa kwa msingi mzuri wa matumizi bora ya takwimu ambazo zinazalishwa na taasisi yetu hii,”alisema Dk Mpango.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, alisema ujenzi wa jengo hilo ni miongoni mwa mikakati ya ofisi yake ya kuboresha miundombinu itakayo wezesha matumizi ya teknoljia ya kisasa katika shughuli za ukusanyaji na uchakataji wa takwimu mbalimbali hatua iliyolenga kupunguza matumizi ya Serikali.

Ujenzi wa jengo hilo ulioanza mwaka 1994 chini ya ufadhili wa Ofisi ya Takwimu ya Sweden (Statistics Sweden) iliyokuwa na ushirikiano na Idara Kuu ya Takwimu chini ya Wizara ya Mipango.

Statistics Sweden kwa mujibu wa kumbukumbu zilizoko waligharamia jengo hili kwa jumla ya Shillingi milioni tano mwaka 1994 na Serikali za Awamu ya Tatu, na Nne ziliendelea na juhudi za kugharamia ujenzi wake hadi lilipofikia kwa gharama ya shilingi 173,386,000.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles