25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Mpango azindua jengo la Mama na Mtoto Sekoutoure

*Asema serikali itaendelea kuboresha hudumza za mama na mtoto

Na Clara Matimo, Mwanza

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango amezindua jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekouture ambalo limegharimu Sh bilioni 12.6 huku akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Uzinduzi huo umefanyika Septemba 13, 2022 katika hospitali hiyo iliyopo wilaya ya Nyamagana mkoani hapa ambapo Dk. Mpango amewataka watumishi wa sekta ya afya kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi na weledi wa taaluma yao huku akiahidi  kwamba serikali itaendelea kuboresha maslahi na mazingira ya kazi.

Alisema kutokana na kuboreshwa kwa huduma katika sekta ya afya nchini kumesaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma bora za mama na mtoto huku akiwataka wazazi kuzingatia maelekezo ya kitaalam yanayotolewa na watoa huduma za afya.

“Mahitaji ya huduma bora ya afya ya mama na mtoto nchini bado ni makubwa kulinganisha na miundombinu ya afya na rasilimali zilizopo kujenga miundombinu zaidi, mojawapo ya changamoto katika sekta hii ni gharama kubwa za matibabu, hata hivyo kwa sasa serikali inaandaa utaratibu mzuri ambao utawezesha kila mwananchi kuwa na bima ya afya kumudu gharama ya matibabu,”alisema Dk. Mpango.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekoutoure, Dk. Bahati Msaki alisema ujenzi wa jengo la mama na mtoto ulianza mwaka 2017 ambapo Juni mwaka huu limeanza kutoa huduma kwa wananchi likiwa na vitanda 261, huduma ya usiri, fursa na heshima  inayompa fursa mama mjamzito kukaa na mwenza au ndugu wakati wa kujifungua.

Alisema mradi huo umegharimu Sh milioni 12.6 huku vifaa tiba kwa ajili ya jengo hilo vikigharimu Sh Bilioni 1.4 ambapo umesaidia kuboresha huduma ya afya kwa wananchi hususan ya mama na mtoto katika mkoa wa Mwanza na mikoa jirani kwani imesaidia kuongeza ari na morali ya utendaji  kazi kwa watumishi pia umepunguza msongamano  wa wagonjwa wodini kwani awali vitanda vilikuwa 140 na sasa vipo 261 na kufanya jumla ya vitanda katika hospitali hiyo kuwa 592.

“Tunategemea kuwa uwepo wa jengo hili utapunguza vifo vya mama wajawazito na mtoto ambapo jengo letu mpaka sasa limeshahudumia akina mama 1,883 na watoto 800,” amesema Dk. Bahati.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula  iliipongeza Serikali kwa kutumia rasilimali ardhi vizuri  kujenga jengo hilo ambalo linapandisha hadhi ya hospitali hiyo ya mkoa, huku akieleza kuwa kukamilika kwake kutawanufaisha wananchi hasa wa kipato cha chini na kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles