30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Mpango ahimiza upandaji miti nchini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango ameutaka Wakala wa Misiti Tanzania (TFS) kuandaa miche mingi ili Watanzania wengi wapate nafasi ya kupata miti katika maeneo mbalimbali nchini.

Maagizo hayo ameyatoa leo Februari 12, 2022 wakati wa zoezi la upandaji wa miti katika barabara ya Chimwaga St. Peter Clever jijini Dodoma, ambalo pia lilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo na Naibu wake, Hamis Hamza Chilo.

“Zoezi hili endelevu tunataka kuibadilisha Nchi yetu hii ni Nchi ya kijani ili hali ya hewa iwe nzuri zaidi tunao uwezo wa kuibadilisha ikawa Nchi nzuri vijana wetu na watoto wao wakaifurahia,”amesema Dk.Mpango.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu kuanzia leo hapa tutakuwa tunafanya mazoezi kama haya mpaka Dodoma itakapokuwa ya kijani kwahiyo niwaombe sana TFS muandae miche mingi Nchi nzima tuipande ya matunda ya mbao kila aina miti dawa Nchi yetu ikawe nzuri tuifurahie,” amesema Makamu wa Rais.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Majaliwa ameagiza zoezi hilo la upandaji miti liwe endelevu nchi nzima lengo likiwa ni kutunza mazingira hivyo ametaka kila mmoja kushiriki katika zoezi hilo.

“Dodoma ni eneo kame lakini sio kame Dodoma  ina ardhi nzuri sana pale unapopata  maji hakuna mmea ambao hautastawi ukija kwenye kampeni inayosimamiwa na Makamu wa Rais ni tukio endelevu na sio kwa Dodoma tu ni Nchi nzima watanzania mnajua  tumekabiliwa na ukame kuanzia mwezi wa nane mpaka Januari kwahiyo tunayosababu ya kupanda miti katika maeneo yote,”amesema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles