Na Ramadhan Hassan,Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel amewataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Akizungumza leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika bonanza la kuchangia damu lillofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na kuhudhuriwa na vikundi vya Jogging kutoka Mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam, Arusha, Njombe, Dodoma na visiwani Zanzibar, Naibu Waziri huyo amewataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ya yasiyoyakuambukiza.
“Tukifanya mazoezi tutaisaidia Serikali katika suala la dawa kwani bajeti ya dawa itapungua kwani wengi watakuwa wapo vizuri katika afya zao naomba sana mfanye mazoezi hapo mnasemaje?amesema.
Naibu Waziri huyo pia amesema Wizara ya Afya itazidi kuhamasisha watu kufanya mazoezi huku akiwataka wafanyakazi wa umma, mashirika na taasisi binafsi kuunda vikundi vya Jogging kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Katika hatua nyingine, Mollel amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengine kwani mahitaji ni makubwa kwa sasa.
“Suala la damu nchi nzima kina mama wetu wanakufa sana sababu ya kukosa damu na hainunuliwi na ipo mwilini mwetu tunahitaji chupa 550,000. Lakini tumepata chupa 300,000 pekee naombeni tuchangie damu, tuokoe maisha ya akina mama. Rais Samia Suluhu alipokuwa akihutubia Bunge suala la mama na mtoto alilirudia mara tatu, hivyo changieni damu,”amesema Mollel.