29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MOLLEL AGEUKA DK. SHIKA BUNGENI


Gabriel Mushi, Dodoma     |  

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Siha, Dk. Godwin Mollel (CCM) leo wameparurana bungeni baada ya Mdee kumwita Dk. Mollel Dk. Shika.

Zogo hilo limeibuka wakati Mdee akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo pamoja na mambo mengine aliishangaa serikali kutenga Sh trilioni moja kununua ndege ilihali kwenye kilimo imetenga Sh bilioni 11.

Mdee amesema katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali ilitenga Sh bilioni 500 na mwaka huu 2018/ 19 imetenga Sh bilioni 495 kununua ndege mbili wakati taarifa ya Msajili wa Hazina na Shirika la Ndege (ATCL) zinaonesha shirika hilo linajiendesha kwa hasara na madeni lukuki.

Wakati Mdee akiendelea kuchangia mjadala huo, Dk. Mollel aliomba kutoa taarifa kwa Spika Job Ndugai huku Mdee akimwambia Dk. Shika kaa chini.

Aidha, Dk. Mollel alipewa fursa na kusema kuwa Chadema kinajinasibu kusimamia miradi yenye ufanisi ilihali kimeshindwa kutumia fedha za ruzuku na michango kujenga ofisi na kumlipa Katibu Mkuu.

Dk. Mollel aliendelea kusisitiza kuwa anakubali kuwa Dk. Shika na ataendelea kuwashika pabaya wabunge wa Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles