26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mengi: Serikali iache kuwashusha thamani vijana

TWITERNa Maneno Selanyika, Dar es Salaam
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi ameitaka Serikali kuacha kuwashusha thamani vijana kuwa hawawezi kufanya jambo lolote.
Alisema badala yake itekeleze sera ya uwezeshaji kwa vitendo kama njia ya kuwakwamua katika lindi la umaskini.
Mengi alikuwa akizindua mradi wa ‘Airtel Fursa’ Dar es Salaam jana, ambao unaendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kuwasaidia vijana kukuza na kuanzisha biashara.
Alisema vijana wengi wamekuwa hawajiamini tatizo ambalo ni kubwa kwa Watanzania wote kutokana na mfumo uliowekwa na viongozi wa Serikali kwa ujumla.
“Serikali ilianzisha sera ya uwezeshaji kwa vijana lakini cha kushangaza tangu mwaka 2004 hadi sasa hakuna chochote kilichotendeka, viongozi hao hao wamewaweka vijana namba mbili badala ya kuwa kuwaweka namba moja.
“Ni jambo la kushangaza kuona viongozi haohao badala ya kuwasaidia vijana wawe namba moja wanabakia kuwaweka namba mbili kwa kusema ‘hamna uthubutu wala hamna fedha’.
“Nataka kila kijana badala ya kusema nataka kuwa tajiri kama Mengi, aseme nataka kuwa tajiri zaidi ya Mengi, pia badala ya kusema siwezi, au haiwezekani, aseme naweza, na inawezekana. Hii ndiyo mbinu ya mafanikio,” alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel, Balozi Juma Mwapachu, aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampuni hiyo ili kujikwamua na umaskini.
Alisema vijana sasa wanapaswa kutazama kwa mapana na kuona fursa ambazo zinaweza kuwasukuma katika maendeleo badala ya kusubiri kuletewa kila kitu na serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso, alisema mradi huo wa fursa una lengo la kuwanufaisha vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles