23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

DK. Mengi amwaga madawati ya milioni 70/-

mengiNA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya IPP Media, Dk.Reginald Mengi ametoa msaada wa madawati  yenye thamani ya Sh milioni 70 kwa  wilaya za Bagamoyo, Pwani   na Handeni, Tanga kuiwezesha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza   Dar es Salaam jana na wakuu wa wilaya hizo  na viongozi wa halmashauri, Mengi alisema msaada huo utasaidia kuondoa changamoto iliyopo katika sekta ya elimu nchini.

Alisema ana imani ushirikiano wa dhati utasaidia kupatikana kwa wingi  madawati hayo ambayo Rais Dk. John Magufuli aliagiza jamii kuchangia kuondoa tatizo la watoto kukaa chini.

“Anayefahamu matunda ya elimu ni taifa zima ni imani yangu madawati yakipatikana na changamoto zilizopo sasa zikatokomezwa kila mmoja atafaidi huduma za wataalam watakaopatikana kwenye fani mbalimbali,” alisema   Mengi.

Alisema wakati umefika sasa kwa viongozi kutumia fursa walizonazo kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu nchini.

Mengi alisema ushirikiano wa dhati kati ya viongozi na wananchi utasaidia kuleta maendeleo nchini katika sekta mbalimbali.

Pia alisema  ni vema viongozi wakaacha uoga wa kutumbuliwa  na badala yake wafanyekazi kwa maslahi ya jamii na taifa Kwa ujumla.

Mengi aliwaahidi viongozi hao kushirikiana nao kwa karibu katika kuendesha kampeni za upatikanaji wa madawati.

Alisema fedha hizo alizozitoa zitumike kununua madawati 500 Kwa wilaya hizo mbili na anaamini atakuwa amesaidia kupunguza kero kwa watoto hao.

 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Husna Msangi alisema wilaya yake inakabiliwa na upungufu wa madawati 752,000.

“Tunashukuru kwa sasa tuna madawati 4,000 hivyo tukipata mengine angalau tutaondoa changamoto iliyopo sasa,” alisema Husna.

Alisema jamii ijitokeze kuiwezesha sekta hiyo ili taifa linufaike na zao la elimu ambalo litatoa wataalam wa fani mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles