30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mayunga: Viwanja 1200, 000 havina hati

mayungaNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Sellasie Mayunga amesema kati ya viwanja 1,816,009, vilivyopimwa kati ya hivyo vyenye hati ni 586,000 tu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam jana kabla ya makabidhiano ya ofisi ya Naibu Katibu Mkuu mpya, Dk. Moses Kusiluka ambaye hata hivyo hakuhudhuria makabidhiano hayo, Dk. Mayunga alisema ufinyu wa bajeti katika wizara hiyo, unachangia kuzorota kwa baadhi ya kazi, ingawa kuna baadhi ya changamoto zimeanza kutatuliwa.

Kuhusu baadhi ya watendaji wa wizara hiyo ambao wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na utovu wa nidhamu na maadili kazini, wamechukuliwa hatua kwa kuwahamishiwa sehemu mbalimbali.

“Changangamoto tuliyokuwa nayo, ni ufinyu wa bajeti zimeanza kutatuliwa…kuhusu watumishi wenye utovu wa nidhamu  ambao wanakuwa na tabia ya kuomba rushwa wamechukuliwa hatua.

“Yale majipu madogo madogo tulishayatumbua, kwa Serikali hii ya awamu ya tano, majipu yote yatatumbuliwa hapa hapa,wasitegemee kuhamishiwa popote,” alisema Dk.Mayunga.

Alimtaka Dk. Kusiluka kuhakikisha anashughulikia mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi  uliopo  Ziwa Nyasa ambao ulianza Mei 3,1967  hadi sasa haujapata ufumbuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles