24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Masaburi alazwa Hospitali Muhimbili

Dk. Didas Masaburi
Dk. Didas Masaburi

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Masaburi amelazwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu, ambayo hata hivyo haijawekwa wazi anasumbuliwa na maradhi gani.

Mmoja wa madaktari wa kitengo cha dharura hospitalini hapo alithibitisha kupokewa kwa kiongozi huyo na kwamba amelazwa katika wodi ya Mwaisela.

“Ni kweli Dk. Masaburi amelazwa hapa Muhimbili wodi ya Mwaisela lakini nakushauri watafute wasemaji au muuguzi wa zamu hao watakupa maelezo zaidi,” alisema.

Akizungumza na MTANZANIA mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo.

“Ni kweli amelazwa hapa hospitalini kwa matibabu lakini sina ruhusa ya kukueleza kwanini amelazwa hapa watafute wasemaji,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Neema Mwangomo alipoulizwa kuhusu kulazwa kwa Masaburi alisema hiyo ni siri ya mgonjwa na watu wake wa karibu.

“Kiongozi au mtu yeyote akilazwa hapa hatuna ruhusa ya kueleza umma pengine hadi mwenyewe aridhie ni haki yake ya msingi, hatuna mamlaka ya kutoa siri ya mgonjwa,” alisema.

Dk. Didas Masaburi alikuwa meya wa jiji la Dar es Salaam wakati wa Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, aligombea ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini aliangushwa na Saed Kubenea wa Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles