29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Dk. Mary Mwanjelwa; Naibu Waziri Utumishi afunguka alivyosoma PhD miaka mitano

Mwandishi Wetu, Kibaha

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa amefunguka jinsi alivyosoma Shahada ya Uzamivu wa Falsafa (PhD) ndani ya miaka mitano ambapo amesema haikuwa kazi rahisi.

Dk. Mwanjelwa amehitimu shahada hiyo leo Alhamisi Novemba 28, katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), katika mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.

Amesema anawatia moyo watu wote kwani elimu haina mwisho hasa ukizingatia yeye ni mbunge, ni Naibu Waziri na ni mama, lakini bado ameweza kufikia malengo ya kumalizia shahda yake hiyo kwa hiyo kujitoa ili kutimiza malengo yake huku akisisitiza kuwa inawezekana.

“Mimi kwa mfano PhD yangu nimeifanya kwa miaka mitano na kidogo, kwa hiyo kila kitu kinawezekana kabisa ni juhudi zako tu na maamuzi yako, determination yako ni wewe mwenyewe ukiamua unaweza.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa

“Kama ni usiku hulali usingizi utajua mwenyewe unajipangaje na majukumu yako ya kifamilia, kikazi, ya wananchi ili uweze kufikia lile lengo lako, na hii ni kwa faida pia ya Watanzania kwa sababu unajua sisi viongozi wengine ni wanasiasa kwa hiyo hii PhD yangu kwa hiyo mimi nasema ninamshukuru sana Mungu ndiye aliyeniwezesha lakini pia ninaamini kabisa itanisaidia katika shughuli zangu za kila siku na kwa Watanzania wote kwa sababu ninapoelimika zaidi na mimi ni kiongozi wa umma maana yake pia ni umma umenufaika,” amesema Dk. Mwanjelwa.

Akizungumzia kuhusu utafiti aliofanya amesema  ilikuwa inahusu utawala bora; “unajua dunia wanazungumzia utawala bora, mahali popote pakishakuwa na utawala bora nchi inakwenda, nchi ina amani.

“Katika jukumu nililopewa mimi ni utawala bora hata baba wa taifa alisema ili nchi iendelee inahitaji vitu vitatu; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora na vyote kwa pamoja ni utawala bora.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles