25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MAHATHIR MOHAMMED: ‘BABA WA TAIFA’ ALIYERUDI MADARAKANI KUOKOA JAHAZI


 NA MWANDISHI WETU, MITANDAONI      |    

MEI 10 mwaka huu, Malasyia imemwapisha mwanasiasa mkongwe na baba wa taifa hilo Dk. Mahathir Mohammed mwenye umri wa miaka 92 kuwa Waziri Mkuu mpya.

Kiongozi huyo wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohamad ameapishwa kuwa waziri mkuu wa saba wa nchi hiyo baada ya ushindi wake kuishtua dunia kwa kuibuka mshindi wa uchaguzi wa Bunge pamoja na kuwa alistaafu muda mrefu.

Dk. Mahathir ameshinda kiti hicho kupitia muungano wa vyama vya upinzani (Alliance of Hope), ambao umefanikiwa kukiondoa madarakani chama tawala cha Baritan National Coalition cha Waziri Mkuu Najib Razak, kilichokuwa kimetawala Malaysia tangua nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1957. Kuchaguliwa kwake kunamfanya kuwa ni kiongozi mkongwe kuliko wote duniani.

Sherehe ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu mjini Kuala Lumpur na kumaliza uvumi uliokuwa unaenezwa kuwa huenda chama cha Barisan National Coalition-BNC kingejaribu kung’ang’ania madaraka.

Wakati akiapishwa Dk. Mahathir alivalia vazi la utamaduni wa Malaysia na kofia ya Kiislamu, aliapishwa na Mfalme Sultan Muhammad, katika tafrija iliyofuata utamaduni wa nchi hiyo.

Kwa upande wake waziri mkuu aliyemaliza muda wake Najib Razak amekubali matokeo na kusema yeye na wenzake katika chama wamekubali uamuzi wa wananchi wa watauheshimu.

Awali ushindi wa Dk. Mahathir Mohammed ulichangia serikali kutangaza mapumnziko ya siku mbili ya kitaifa kwa siku ya Alhamis na Ijumaa.

Kwanini imekuwa rahisi Dk. Mahathir kushinda?

Zipo sababu mbalimbali zilizochangia kuangushwa Razak, lakini kubwa zaidi ni sita, ambazo zimemnyamzisha hata waziri Razak mwenyewe.

Kwanza ni hali mbaya ya ulinzi na usalama nchini Malaysia ambapo kumeshuhudiwa mapigano na utengano mkubwa baina ya jamii zao. Kumekuwa na mgogoro baina ya Waislamu na Washia, hali ambayo ilisababisha matatizo ya kijamii, ulinzi na usalama. Kumeshuhudiwa kupanda kwa cha mapigano ya kikabila nchini humo.

Pili, ni kuvurugika kwa uchumi wa Malasyia ambako kumechangia kuangushwa kwa waziri huyo kwa sababu Dk. Mahadhir ametumia kama nyenzo ya kuombea kura na kuibuka mshindi. Wananchi wana hali mbaya ya kiuchumi; kuanguka biashara ya nyumba.

Kwa mujibu wa Naibu waziri wa fedha wa serikali iliyoangushwa, Lee Chee Leong alisema ni asilimia 40 ya biashara ya nyumba imefanyika sawa na mauzo ya nyumba 20,807.

Nayo ripoti ya Free Malaysia Today (FMT) ya Novemba mwaka 2017 ilikariri kampuni ya uuzaji wa majengo ya Ernest Cheong PTL kwamba uwezo wa kifedha wa wananchi uliporomoka kupindukia kuliko kipindi cha miaka 10 iliyopita.

“Kuna majengo yenye thamani ya fedha ya Malayasia Bilioni 16 yanasubiri wanunuzi. Lakini hakuna mtu mtaji w akutosha. Sababu kubwa ni kwamba watu hawana fedha mikononi.” ilisema taarifa hiyo

Kisheria nchini Malaysia wanunuzi wa majengo wanahitaji kulipa asilimia 1 ya malipo ya awali, lakini kutokana na hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa fedha ilisababisha kupanda hadi asilimia 10 ya malipo ya awali kwa mwaka 2017. Hadi sasa wauzaji wa majengo wanatumia asilimia 10 kwa sababu ongezeko la ugumu wa kuuuza na kununua.

Aidha, wanunuzi wa majengo wakishindwa kuuza angalau kwa asilimia 40, wanajiweka katika hatari ya kukosa mikopo kutoka benki. Vilevile benki haziwezi kutoa mikopo isiyofanya vizuri sokoni (Non-performing Loans).

Kwa mfano bei ya nyumba ilishuka kutoka Ringgit (fedha ya Malaysia) 500,000 sawa na dola za Marekani 125,060 mwaka 2017 hadi ringgit 300,000 sawa na dola za Marekani 75,036 kwa mwaka 2018. Hii ni hali ambayo wananchi walishindwa kuvumilia hivyo uamuzi wao ukachukuliwa ndani ya sanduku la kura kumrejesha ‘Baba wa Taifa’ hilo ili kuokoa jahazi.

Tatu, Malayasia ingawa inasifika kwa tatizo dogo la ajira lakini limetumiwa na wapigakura kuiangusha serikali . Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zikiikariri ripoti ya Benki Kuu ya Malaysia inaonyesha kuwa asilimia 12 ya soko la ajira kwa mwaka 2016 nchini humo limechukuliwa na wageni.

Uhaba wa ajira kwa wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kimeongezeka hadi asilimia 10.8 mwaka 2017. Idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu imeongezeka kwa kasi tangu mwaka 2011. Licha ya Malayasia kuwa nchi yenye kiwango kidogo cha uhaba wa ajira, ambapo asilimia 3.30 ya wananchi kitaifa hawajaajiriwa.

“Mahitaji ya fursa ya ajira ni changamoto kubwa kwa utawala mpya wa Dk. Mahathir kwa sababu ajira imekuwa ikichukuliwa kama msingi wa hoja za kampeni za uchaguzi na ustawi wan chi hususani maeneo ya miji na mijini,” anasema Profesa Awang Azman Awang Pawi w Chuo Kikuu cha Malaya .

Nusu ya kwanza ya mwkaa 2017 biashara ya nyumba ilikuwa mbaya na kusababisha nakisi kwa mapato ya serikali.

Jambo la nne, Waziri Mkuu Najib Razak ameshindwa kufuatia kashfa nyingi zinazomkabili. Razak amehusishwa na kashfa ya kudaiwa kujipatia kiasi cha dola za Marekani 700 kutoka Taasisi moja ya maendeleo ya Malaysia na mamlaka zinaendelea kuchunguza kashfa hiyo. Tuhuma za ufisadi na ulaji wa rushwa kupindukia zimewachosha wananchi kiasi kwamba njia pekee iliyokubalika ni kuondoa utawala mzima.

Sababu ya tano, serikali imeangushwa kwa kuwa ilishindwa kutatua matatizo ya wananchi wa kawaida, ambao wamekuwa wakilipwa kipato kidogo mno.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa Bloomberg imeeeleza kuwa matatizo ya kipato kidogo, ingawa linahusishwa kuanguka biashara za majengo, lakini hii ni mojawapo na imegusa moja kwa moja wapigakura. Imeelezwa kuwa kukosa kuzalisha ajira, Malaysia inatakiwa kubadilisha mfumo wake wa uzalishaji.

Bloomberg wamemkariri Gavana wa Benki Kuu Muhammad Ibrahim, katika taarifa yake ya Machi mwaka huu. Umesema kitendo cha kusafirisha wazalishaji wenye ujuzi mdogo kwa malipo madogo yenye lengo la kuinua uchumi, ni chanzo cha kushuhudia taifa hilo likikabiliwa na mishahara duni isiyomithirika.

“Tatizo la kuajiri wafanyakazi wenye ujuzi mdogo lilianza miaka 1990 na baadaye kurasimishwa lengo likiwa ni kupandisha kiwango cha uchumi wa nchi.”

Takwimu za Benki Kuu ya Malayasia zinaonyesha kuwa wafanyakazi haramu (wasio na vibali) kutoka ng’ambo ni asilimia 12 wakiwa ndiyo msingi wa uzalishaji mwaka 2017baada ya kupungua kutoka asilimia 16.1 ya mwaka 2013. Lakini pia wanaamini wafanyakazi hao watapandisha hadi asilimia 40 ya uzalishaji, jambo ambalo halijatimia naserikali imeangushwa.

Kwa upande wake Dk. Mahathir na Muungano wa chama chak cha Pakatan Harapan umeahidi kuzalisha ajira milioni moja pamoja na ongezeko la mishahara angalau Ringgit 2,500 sawa na dola za Marekani 636.

Sababu ya sita, Chama cha Barisan Nasional (BN) kimetawala Malaysia kwa zaidi ya miaka 60. Wafuasi wa Dk. Mahathir wanaendelea kusherehekea ushindi huo licha ya kiapo kukamilika. Lakini ujumbe mzito wa sauti ya wananchi nchini Malaysia ulianza kutolewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008.

Ulikuwa uchaguzi wa kwanza tangu mwaka 1969 ambapo chama cha BN kilipoteza theluthi ya Bunge la Taifa. Kushindwa huko kunatokana na wananchi kutoridhishwa na uongozi wa chama hicho, huku migogoro ya kijamii ikishika kasi.

Kumekuwa na mgogoro baina ya jamii zenye asili ya China na India nchini Malayasia, hali ambayo imechangia kugawanywa kwa kura kila unapowadia Uchaguzi Mkuu. Licha ya ahadi iliyotolewa na Najib Razak kutekeleza sera ya “Malayasia Moja” bado hakufanikiwa. Mpango huo umetumika pia kama nyenzo ya kumchapa kwenye sanduku la kura hivyo kuiangusha Serikali nzima.

Makundi ya kijamii yenye kuibua migogoro yameshamiri kwa kiasi kikubwa, hivyo Dk. Mahathir ametumia hoja hii kuwaunganisha wapigakura wengi bila kujali jamii zao, huku akiahidi kumaliza migogoro pamoja na kuhakikisha utawala wa sheria unachukua kasi.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, William De Cruz, katika andiko lake kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Malaysia amewapongeza wananchi kwa madai kuwa wameleta mabadiliko bila kutumia silaha yoyote ya moto zaidi ya sanduku la kura dhidi ya serikali iliyochoka na kushindwa kuongoza nchi.

“Muungano wa Serikali uliohodhi haki za watu mbalimbali nchini Malaysia kwa miaka 61 umeondolewa katika uchaguzi wa 14 wa kidemokrasia, kuanzia mhimili wa Mahakama, Jeshi la Polisi, mifumo ya vyuo vikuu, Tume ya uchaguzi, Bunge, matabaka na dini zote,”

“Malaysia imeonyesha upekee kwenye suala la uchaguzi, na wametia hamasa nchi zingine. Wameirudisha demokrasia kwenye mstari wake kwa sababu ilikuwa imetumbukia shimoni, kwahiyo Malaysia itajengwa upya katikati ya makundi ya kijamii, demokrasia na misingi ya waasisi wa taifa na wazalendo.

Kwanini Dk. Mahathir amepewa sifa ya kuwa Baba wa Taifa?

Dk. Mahathir Mohammed amewahi kuongoza Malaysia kwa kipindi cha miaka 22. Alikula kiapo cha kwanza kuwa waziri mkuu wa Malaysia mwaka 1981 akiwa na miaka 56. Mara baada ya kuingia madarakani mwaka huo aliwachilia huru wafungwa 21 wa kisiasa walioweka kwa mari ya Sheria ya Usalama wa Taifa, akiwapo mwandishi wa habari Samad Ismail na naibu waziri wa zamani Abdullah Ahmad.

Mwaka 2007 Dk. Mahathir alijitoa katika chama tawala baada ya aliyekuwa waziri mkuu, Abdullah Badawi kukataa wito wa kujiuzulu uliotolewa na mtangulizi wake huyo.

Mahathir Mohamad ambaye alimteua Badawi kuwa mrithi wake mwaka 2003 alisisitiza kwamba hatorudi kwenye chama hicho cha Muungano wa Taifa wa Wamalay (UMNO) hadi hapo waziri mkuu huyo atakapong’atuka. Hilo halikufanyika naye akajitoa. Dk. Mahathir Mohammed anachukuliwa kama baba wa taifa. Sauti yake huwa ya kitaifa (Statesman).

Ahadi zake

“Tumedhamiria kukuza uchumi wa Malaysia kwa msaada wa wawekezaji wa ndani na nje. Tutajitahidi kuimarisha thamani ya fedha yetu kadiri inavyowezekana. Tumedhamiria pia kuhakikisha tuna imani na wawekezaji katika mikakati yetu na yao. Tunasuka serikali nzuri, kwa kuhakikisha tunafuata Katiba inafuatwa na utawala wa sheria unachukua nafasi yake katika nchi hii. Sisi hatujaingia madarakani kwa madhumuni ya kupambana na waziri mkuu Najib Razak.” Alisema Dk. Mahathir mara baada ya kuapishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles