31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli umeingia kwenye historia

SARAH MOSSI – DAR ES SALAAM

WIKI kadhaa nchi yetu imeshuhudia inaingia kwenye historia baada ya Rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji kati ya Tanzania na Misri ambao umesubiriwa kwa zaidi ya miaka 40.

Tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi wote wa Kitaifa akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na takriban mawaziri wote lilishuhudiwa pia na wananchi wote wa ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari.

Ni chukue nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wabusara na wa dhati kuamua kuufufua mradi huu na kuuendelea ambao kwa maneno yake mwenyewe aliwaambia waliohudhuria hafla ya utiaji saini kwamba mradi huo ulianza tangu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Nyerere lakini ulikwama utekelezaji wake.

Mradi wa umeme wa Bonge la Mto Rufiji si tu utawanufaisha Watanzania kwa maana ya kupungua kwa gharama za kununua umeme lakini pia mradihuo  utakuza uchumi wa Taifa letu kwa sababu utakapokamilika nchi yetu itaingia kwenye historia ya kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zinazouza nishati hiyo kwa nchi nyingine.

Wapo baadhi ya watu waliupinga mradi huo kwa madai kuwa utaharibu mazingira lakini kwa mujibu wa timu ya wataalamu inasema mradi huo utakapokamilika utasaidia pia kutunza mazingira katika Hifadhi ya Selous.

“Mradi huu umepigwa vita sana kwa hiyo sishangai kama mawazo haya ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere tangu mwaka 1970 leo ndiyo tunakuja kuweka saini zaidi ya miaka 40, nilijua matatizo waliyokuwa wanapambana nayo.

“Nafahamu wapo wanaosema mradi huu utaharibu mazingira, hiyo si kweli hata kidogo ninavyojua mradi huu utasaidia kutunza mazingira. Kwanza ni kwa sababu umeme wa maji ni rafiki wa mazingira, pili eneo la kutekeleza mradi huu ni dogo ambalo ni asilimia 1.8 hadi 2 ya eneo zima la Selous.”

Nimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake huo na kuamua kutosikiliza kelele za watu waliokuwa wakiupinga mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme kwa miaka 60 na gharama za kuzalisha umeme wa maji zikiwa nini ndogo kuliko zingine, gharama za kuuza pia zitakuwa nafuu kwa hiyo ukikamilika umeme utashuka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa na Rais Magufuli siku ya kusaini mradi huo ni kwamba bei ya umeme kwa nchi yetu ni kubwa kuliko nchi zingine ambapo uniti moja inauzwa kwa dola za Marekani senti 10.7 wakati Misrini senti 4.6, Korea ya Kaskazini ni chini ya senti 8, China nayo ni hivyo hivyo chini ya senti 8.

Afrika Kusini ni senti 7.4, India ni senti 6.8, Ethiopia senti 2.4.

Ukiziangalia takwimu hizi utabaini kwa hali hii  ndiyo inafanya gharama za uzalishaji nishati hiyo kuwa juu kwa sababu gharama za umeme ziko juu.

“Mradi huu utakapokamilika tutauza umeme kwa bei ya chini, uzalishaji kwenye viwanda vyetu itakuwa kwa bei ya chini na tutaweza kushindana kwenye soko la kimataifa,”alisema Rais Magufuli.

Katika hili Watanzania tunapaswa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukaa na kubuni chanzo mwafaka cha kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa chini na kuamua kuufufua mradi huo ulio kwama kwa miaka 40 sasa.

Kuhusu Hifadhi ya mazingira, kutokana na umuhimu wa mradi huo wa Taifa, Rais Magufuli alisema ukikamilika utapunguza ukataji wa miti kwa sababu utafiti uliofanyika mwaka 2015, mgawanyo wa matumizi ya aina ya nishati ya kuni na mkaa ni asilimia 92, petrol asilimia 7 na umeme asilimia 1.

“Kwa mujibu wa utafiti huo, matumizi ya mkaa yanakadiriwa kuwa ni tani milioni 2.3 kwa mwaka na inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030.

“Ili kuzalisha tani moja ya mkaa kwa kutumia matanuru ya kienyeji zinahitaji tani 10 mpaka 12 za miti ili upate tani moja ya mkaa, hii maana yake ni kwamba  milioni 2.3 za mkaa tunazotumia kwa mwaka zinahitaji milioni 23 hadi tani milioni 27 za miti.

“Utafiti unaonesha kwa kila miti 18 inatoa magunia 26 ya mkaa yenye kilo 53 zitatumia miti milioni 30. Hivyo basi kukamilika kwa mradi huu utasaidia kuokoa idadi kubwa ya miti na hivyo kutunza mazingira yetu ndiyo maana nasema huu mradi ni rafiki wa mazingira kwa sababu utaokoa miti inayokatwa kwa ajili ya mkaa na kuni,” alisema Dk. Magufuli katika hafla hiyo.

Hivyo basi ningewaomba watu wa mazingira na watunza mazingira nchini kuunga mkono mradi huo mkubwa wa kihistoria nchini kwa sababu utatunza mazingira na kuinua uchumi wa Taifa letu.

Kwa wakazi waishio jirani na unapotekelezwa mradi huo,chonde chonde nawaomba kuunga mkono juhudi hizo za Rais na hatutarajii kutokea au kusikia hitilafu zozote zile wakati mradi huo ukitekelezwa.

Wao ndio watakuwa walinzi wa mradi huo wakati ukitekelezwa, wao watakuwa wasaidizi wa wataalamu wetu wa mradi huo ili hapo baadaye historia iwakumbuke kwa mema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles