22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli: Nitafuta Wiki ya Maji

magufuli1Na Bakari Kimwanga, Morogoro

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao, Serikali yake haitakuwa na maadhimisho ya Wiki ya Maji.

Dk. Magufuli, aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni wa kuomba kura za kuchaguliwa mjini hapa.

Wiki ya Maji kitaifa huadhimishiwa Machi 16 hadi 22 kila mwaka, ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa huzindua miradi ya maji vijijini na mijini na kuweka mawe ya msingi.
Kwa mwaka huu, wiki hiyo iliadhimishwa kitaifa mkoani Mara.

Dk. Magufuli alisema inashangaza kuona watu wanafanya maadhimisho hayo, huku mamilioni ya fedha yakitumika, na wananchi wakiendelea kukosa maji mijini na vijijini.

Alisema hakuna haja ya kuwa na maadhimisho hayo, kwa sababu yanaonekana hayana faida kwa wananchi.
“Mimi nimeomba urais sio kwa majaribio, ninajua matatizo ya Watanzania, ndiyo maana nasema na ninajua hapa hakuna maji, kule juu wanatafuta fedha kwa maadhimisho ya Wiki ya Maji wakati watu hawana maji.

“Kama mtanichagua, Serikali yangu ya awamu ya tano itafuta maadhimisho haya, fedha nyingi zinatumika.
“Kuchimba kisima kimoja hakizidi Sh milioni 25 na Waziri wa Maji nitakayemteua atakuwa na kazi ya kuleta maji na si kila siku tuko kwenye mchakato.

“Akiwa na lugha hii itabidi akae pembeni ili akajichakatue mwenyewe, sikubali hata kidogo. Kikubwa nawaomba mniamini na mnichague ili nianze kazi hii kwa kasi ya kuwatumikia,” alisema Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles