24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk.Kiruswa: ‘Wafanyabiashara wa Madini Jasi fuateni bei elekezi ya Serikali’

Na Clara matimo, Lindi

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa amewataka Wafanyabishara wa Madini ya Jasi kufuata bei elekezi iliyopangwa na Serikali huku akitoa onyo kwa watakaokiuka kwani kufanya hivyo ni kuwanyonya wachimbaji wa madini hayo.

Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa akizungumza na wanawake wachimbaji wa madini( hawapo pichani) wakati akifunga kongamano hilo.

Pia, ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kufanya tafiti katika maeneo ya uchimbaji madini Mkoani Lindi ili kuwasaidia wachimbaji wa madini waliomo ndani ya mkoa huo kuepuka uchimbaji wa kubahatisha.

Dk. Kiruswa ametoa onyo na agizo hilo Mei 31,2023 wakati akifunga Kongamano la Chama cha Wanawake katika Sekta ya Madini 2023 (TWIMMI) lililofanyika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na kukutanisha zaidi ya wanawake 700 kutoka mikoa mbalimbali ya Kimadini nchini ikiwemo Dodoma.

Alisema Serikali haitawavumilia wafanyabiashara wanaokiuka bei elekezi ya madini hayo maana lengo lao ni kujinufaisha wenyewe na kuwanyonya wachimbaji wa madini hayo wakati nia yake ni kila mtu kwa nafasi yake anufaike na rasilimali hiyo.

Aidha Dk. Kiruswa aliwashauri wachimbaji wanawake wa madini nchini kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo ikiwemo GST ili wafanye uchimbaji wenye tija waweze kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanzidata wa GST, Terrence Ngole amewasisitiza wachimbaji wa madini wanawake kutumia taarifa za tafiti zinazotolewa na GST ili kuongeza tija na kuchimba kwa faida pasipo kubahatisha.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alitoa wito kwa wachimbaji wote nchini kushiriki Kongamano la Madini la Mkoa wa Lindi linalotarajiwa kufanyika Juni 2023 mkoani humo ili waweze kubadilishana fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao.

Baadhi ya wanawake wachimbaji wa madini walioshiriki kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja

“Nashukuru sana TWIMMI kwa kuandaa kongamano hili mkoani kwetu Lindi lililoambatana na maonesho ya madini hakika naamini wachimbaji wetu ndani ya mkoa huu wamenufaika kwa kutambua fursa mbalimbali ambazo zitawanufaisha naendelea kuwasihi wachimbaji wote wa madini nchini waje hapa Lindi Juni mwaka huu kushiriki kongamano la madini mk,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles