Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete amesema kama vijana wa Kitanzania hawafanyi vizuri kwenye masomo ya Sayansi kuna haja ya kukutana na Wahadhiri wa vyuo vikuu kujadili kwanini hawafanyi vizuri kwenye masomo hayo ili waweke sawa changamoto hiyo.
Dk. Kikwete amebainisha hayo Agosti 31, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla kutambua mchango wa wadau wa sekta ya elimu kwa kufanikisha upatikanaji wa Dola za Kimarekani milioni 50 kupitia “GPE Multiprier Grant” uliofanyika katika ukimbi wa Diamond Jubilee huku ukihusisha viongozi mbalimbali wa serikali, dini, sekta binasfi na wadau wa elimu.
Amesema utaratibu huo wa kukutana unatoa fursa nzuri kwa wadau kushirikiana kuendeleza sekta ya elimu nchini.
“Kutokana na hali hii kuandaa mkakati wa kujadili na kuelezena changamoto zinasababishwa kwanini wanafunzi wanafeli ili kuweka mikakati sawa ya kwetu tuweke sawa kazi ibaki kwa wanafunzi,” amesema Dk. Kikwete.
Amesema Shirika la GPE limeanzishwa miaka 20 iliyopita ikiwa lengo ni kusaidia elimu nchi zenye mapato ya chini, vita na Tabia ya nchi.
Amesema GPE inajihusisha na elimu kuanzia shule ya awali msingi na sekondari na kuhakikisha wanapata elimu na lazima iwe bora na usawa wa jinsia na uheshimiwe.
Aidha, Dk. Kikwete amasema kuchangia elimu kwa maslahi ya Taifa watu walivyochangia kunawaleta pamoja wadau wa elimu ndani na nje ya nchi.
Dk. Kikwete ni Mwenyekiti wa Bodi ya GPE yenye wajumbe 40 ambapo nchi 88 wamejinga na GPE Desemba mwaka huu na wanatarajia kufanya mkutano nchi Visiwani Zanzibar.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kazi kubwa ya hafla hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali kuchangia sekta ya elimu.
“Sera ya elimu na mafunzo mwaka 2014 tuliangalia mambo ya msingi ambayo yamewekwa hayajafanyiwa kazi ikiwemo elimu ya msingi itakuwa miaka sita na minne sekondari jumla 10 anamaliza shule akiwa na miaka 16,”amesema Prof. Mkenda.
Amesema sera ya mwaka 2014 wapo kwenye mchakato watapeleka ipitishwe bungeni na mapendekezo mwezi ujao yatapishwa na baade kutangazwa.
Profesa Mkenda amesema lengo kubwa ni kuboresha elimu nchini na katika kuendeleza elimu kuna hitaji gharama wadau mbalimbali wakutane kuchangia.