31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kijazi: Mwaka 2019 ulivunja rekodi ya mvua

Mwandishi Wetu -Dar eS Salaam

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwaka 2019 umeweka rekodi na  kushika nafasi ya nne kwa kuwa na kiasi cha mvua nyingi tangu mwaka 1970

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alipokuwa akitoa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya hali ya hewa wakati wa kikao cha Bodi ya TMA.

Akizindua ripoti hiyo, Dk. Kijazi alisema mwaka 2019 umechukua nafasi ya nne kwa kurekodi kiasi cha mvua nyingi tangu mwaka 1970 kiwango ambacho ni kikubwa sana kutokea.

Alisema kiwango cha mvua kwa mwaka 2019 kilikuwa na wastani wa milimita 1283.5 sawa na asilimia 125 ya wastani wa mvua ya muda mrefu, 1981-2010, na kuongeza kuwa  kiwango hicho ni cha  zaidi ya wastani wa mvua ya muda mrefu kwa milimita 256.5.

Alisema katika historia, mvua ya mwaka 2019 imechukua nafasi ya nne kwa wingi kati ya miaka iliyopata mvua nyingi zaidi tangu mwaka 1970 ambapo miaka iliyokua na mvua nyingi zaidi tangu mwaka huo ni 1982, 1997 na 2006.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza joto la nchi limeendelea kuongezeka kwa kiwango cha juu kuanzia mwaka 1995, ambapo joto la usiku limeongezeka zaidi ilikilinganishwa na joto la mchana ambapo kwa wastani joto kubwa kupita viwango vya kawaida (35 °C) limekuwa likiripotiwa katika miezi ya Januari, Februari na Machi.

“Hasa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa nchi ambayo ni pwani ya kaskazini na maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki huku Joto la chini kupita kawaida (5 °C) limekuwa likiripotiwa zaidi katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi hasa miezi ya Juni, Julai,” alisema

Pamoja na hayo taarifa za ripoti zitolewazo zimekuwa zikitumika pia kuchangia ripoti za namna hii zinazoandaliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Aidha, Dk.Kijazi aliwashauri wadau wa sekta wa mbali kutumia taarifa zilizopo kwenye ripoti hiyo kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi katika kukuza nchi na jamii kwa jumla katika tabza kilimo, ujenzi maendeleo ya viwanda na nyingine.

Awali kabla ya kuwasililishwa kwa ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang’a,  alisema ripoti hizo zimekuwa zikitolewa tokea mwaka 2011 hadi 2019 ambapo lengo kubwa ni kukuza ufahamu na uelewa kwa jamii, wadau na watoa maamuzi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

“Tathmini za ripoti hizi huonesha taarifa za kina za uchambuzi wa hali ya hewa na madhara yake na kuziweka katika mtazamo wa kihistoria,” alisema Dk. Chang’a. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Buruhani Nyenzi, aliipongeza Menejimenti ya TMA kwa kutoa taarifa hiyo kwani ilielezwa kwamba ni nchi mbili tu Afrika ambazo zinatoa taarifa hizo ikiwemo Tanzania na Ivory Coast

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles