26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KIGWANGALLA AFANYIWA UPASUAJI, ASEMA YUPO ‘FIT’ 

NA WAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla, amefanyiwa upasuaji wa kwanza katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu, Mgongo, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI), kutibu mkono wake ambao ulivunjika katika ajali aliyoipata Agosti 3, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi, alisema hali ya afya ya Dk. Kigwangalla baada ya upasuaji huo inaendelea kuimarika.

“Madaktari wetu walimfanyia upasuaji Agosti 12, mwaka huu, hajambo, anaendelea vema… ni wito wetu kwa Watanzania kwamba waendelee kumwombea ili aweze kurejea katika majukumu yake ya kulitumikia taifa,” alisema.

Akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, alipomtembelea wodini mapema jana, Dk. Kigwangalla alisema hivi sasa yupo ‘fiti’.

“Afya yangu inazidi kuimarika, jana (juzi) nimeweza kufanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa miguu kutoka ghorofa ya kwanza hadi ghorofa ya sita nilipolazwa, ikiwa ni siku ya 14 sasa tangu nilipopata ajali ya gari mkoani Manyara,” alisema.

Alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwani aliweza pia kufanya mazoezi hadi eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambako aliwahi kusoma.

Katika ajali hiyo, Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Hamza Temba alifariki dunia na kuzikwa huko nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro.

Habari hii imeandaliwa na ERICK MUGISHA (DSJ), FRANK PETER KAGUMISA (SAUT) na VERONICA ROMWALD

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles