29.3 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

DK. KIGWANGALA AWAPA USHAURI WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuisaidia Serikali kuandaa bajeti ya wizara hiyo.

Kauli hiyo aliitoa juzi mjini hapa, wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.

Katika kikao hicho uongozi wa wizara, idara kuu ya maendeleo ya jamii, uliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya 2016/2017 na kufanya mapitio ya bajeti na mpango wa mwaka 2017/18.

Katika maelezo yake, Dk. Kigwangala alisema ili kufikia malengo, wanahitaji kuwa na mipango na bajeti inayozingatia utekelezaji wa vipaumbele vilivyowekwa kupitia wataalamu wa idara kuu.

“Kwa kutambua hilo, bajeti ya idara kuu ya maendeleo ya jamii imeandaliwa kwa nia hiyo na pia inaakisi sera, mipango, mikakati ya Taifa, ilani ya uchaguzi ya chama tawala na mikataba ya kikanda na kimataifa.

“Pamoja na hayo, lazima watumishi mfanye kazi kwa bidii na maarifa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema Dk. Kigwangala.

Wakati huo huo, naibu huyo aliitaka wizara hiyo kuendelea kutoa motisha kwa watumishi wanaowajibika, wabunifu na wenye maadili mema ili kuwa kichocheo cha ubunifu, tija na ufanisi sehemu ya kazi.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga, alisema wajumbe wa baraza la wafanyakazi watajadili bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,631FollowersFollow
542,000SubscribersSubscribe

Latest Articles