26.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Dk Kalemani: Tanesco wakatieni umeme wadaiwa sugu wote

 MWANDISHI WETU -DODOMA

WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani, ameliagiza Shirika la Umeme nchini ( TANESCO) kuendelea kukata umeme kwa wadaiwa sugu ili kukusanya mapato zaidi na kulipa madeni ya shirika hilo.

Dk. Kalemani alisema hayo, jijini Dodoma alipokutana na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO, kuzungumzia tathimini ya miaka mitano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kiuo cha kupoza na kuzambaza umeme cha Zuzu. 

Dk. Kalemani aliiagiza TANESCO kulipa madeni inayodaiwa na kutoongeza madeni mapya, vilevile wadaiwa sugu wakumbushwe madeni yao na endapo hatawalipa, wakatiwe umeme. 

“TANESCO inadaiwa madeni makubwa pia yenyewe ina wateja wengi sana ambao ni wadaiwa sugu wanaodaiwa fedha nyingi na hawalipi, zimo taasisi, mashirika ya umma na binafsi na watumiaji wa kawaida, ninawaagiza nendeni mkawakatie umeme. Narudia tena mkakate umeme, mkishaukata, wahusika watalipa na wataonyesha ushirikiano tofauti na kumdai kawaida tu”, alisema Dk. Kalemani.

Kuhusu wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme, Dk. Kalemani aliitaka TANESCO, bodi yake na watendaji wa Wizara ya Nishati, kushirikiana kutafuta njia sahihi naya kisasa ya kubaini wizi wa umeme unaofanywa na watu wasiowaaminifu na kusababisha hasara kwa shirika na kupoteza mapato ya taifa.

Aidha aliwataka kuendelea kufanya tathmini na uwiano wa gharama za kutengeneza nguzo za zege na zinazotumika sasa ili kuangalia uwezekano wa kutumia nguzo za zege katika maeneo yote nchini lakini kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwataka TANESCO kuangalia uwezekano wa kutoa zawadi kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa za siri kuhusu wanaohujumu na kuiba umeme.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dk. Alexander Kyaruzi, aliishuruku Wizara ya Nishati kwa kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao na kuyafanyia kazi yale waliokuwa wakiishauri wizara hiyo, katika kipindi chote cha miaka mitano.

Dk. Kiyarunzi, alikiri kwa kuwa kazi ya kusambaza umeme si jambo jepesi, hivyo wanajivunia kuona maendeleo makubwa katika sekta ya nishati ya kuongeza wigo wa usambazaji wa umeme vijijini, kujenga miradi mikubwa ya kuzalisha, njia za kusafirisha na kusambaza umeme pamoja na vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini.

Awali kabla ya kufanyika kwa kikao hicho, Uongozi wa Wizara na Wajumbe wa Bodi hiyo walifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa Kituo kikubwa zaidi nchini cha Kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles