Na WALTER MGULUCHUMA,KATAVI
Waziri wa Nishati, Dk. Medadi Kalemani amezindua mradi wa REA, awamu ya tatu mkoani Katavi ambao utekelezaji wake utatumia ziaidi ya Sh bilioni 39.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, alisema REA awamu ya tatu katika mkoa huo itafaidisha vijiji 116 ambavyo havina huduma ya umeme.
Alisema umeme huo utasambazwa katika vijiji vyote na Kampuni ya China Railway Constration Company Limited iliyopewa mkataba wa miezi 24 kukamilisha mradi huo.
Dk. Kalemani alimwagiza mkandarasi wa mradi huo kusambaza umeme maeneo yote ya taasisi za serikali.
Pia alimtaka kusambaza umeme kaya kwa kaya bila kubagua nyumba hata kama ni ya nyasi.
Alisema mradi huo unatarajia kuwafikia wananchi 10,000 na utakuwa endelevu .
Aliwaonya watu wenye tabia ya kuharibu miundombinu ya umeme kaacha tabia hiyo kwa sababu inasababisha hasara.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla, alisema mkoa huo bado unao mahitaji ya umeme.