23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

DK. KALEMANI AAGIZA REA KUUNGANISHA UMEME VIJIJI VITATU KILA WIKI

Na Amina Omar, Tanga

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki.

Pia amesema kuwa wizara yake haitaongeza muda wa mkataba kwa wakandarasi watakaoshindwa kukamilisha kazi kwa wakati.

Dk. Kalemani amesema hayo leo Jumatatu Machi 26, wakati akizindua mradi wa umeme katika Kijiji cha Magumbani Kitongoji cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga.

“Wakandarasi hakikisheni mnatoa kipaumbele cha kuunganisha umeme katika taasisi za serikali kwenye eneo ambalo mradi upo badala ya kusubiri hadi mradi umeshakamilika ndiyo mnaanza maombi ya kuunganishiwa umeme,” amesema.

Vile vile Waziri huyo amelitaka Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kuhakikisha wanasimamia zoezi la uunganishaji umeme ili kuepukana na vishoka wanawalaghai wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark amesema changamoto kubwa iliyopo katika wilaya hiyo ni eneo kubwa kukosa huduma ya nishati ya umeme hivyo kuchangia kuchelewesha shughuli za maendeleo.

“Licha ya kujitahidi kuchimba bwawa kubwa la maji lakini tumeshindwa kusambaza huduma ya maji katika maeneo ya karibu na wananchi kutokana na kukosa nishati ya umeme,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles