24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Jingu: Shughuli za wanawake zimewezesha uchumi wa kati

LEONARD MANG’OHA, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. John Jingu, amesema shughuli mbalimbali ambazo zinafanywa na wanawake kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri nchini zimeiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati.

Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea jijini hapa.

Dk. Jingu alisema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini, ikiwamo upatikanaji wa mitaji kupitia benki pamoja na kuweka afua mbalimbali kuwawezesha wale wasioweza kupata mikopo katika sekta ya benki kuipata kwa kutumia utaratibu wa halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa wanawake, vijana na wenye ulemevu.

Alisema kuwa hadi sasa tayari halmashauri zimetoa Sh bilioni 39.7 ya mikopo hiyo kwa makundi hayo kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi na kwamba zaidi ya wanawake 800,000 wamewezeshwa.

Dk. Jingu alisema shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanawake zimechangia kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati ambao ulitangazwa na Benki ya Dunia hivi karibuni.

“Serikali imefanya mambo mengi kuhakikisha uchumi wa viwanda unakuwapo nchini. Baadhi ya mambo ambayo imeyafanya ni kuondoa kero katika mfumo wa kodi na tozo mbalimbali ambazo zilikuwa ni kero zimeondoshwa.

 “Lakini mfumo wa kutoa vibali na leseni mbalimbali umerahisishwa, lakini pia ufanyaji maamuzi umekuwa wa haraka kuondoa urasimu usiokuwa na sababu, soko pia lipo na Watanzania wamehamasika wanatumia bidhaa za ndani na mazingira ni mazuri,” alisema Dk. Jingu.

Alisema uchumi wa viwanda unahitaji mfumo mzuri wa kisera na kisheria wa kikodi na kwamba Serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri zaidi.

Kuhusu upatikanaji wa soko la bidhaa zinazozalishwa, alisema kuwa Tanzania bado ina soko kubwa la ndani Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla kupitia mikataba mbalimbali ambayo nchi imejiunga.

Dk. Jingu aliwataka wafanyabiashara nchini kujitokeza kuwekeza katika kutengeneza dawa, vifaa pamoja na bidhaa zingine zinazohitajika zaidi ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

“Tutaendelea kuwaomba wawekezaji wakubwa kutoka nje kuja kuwekeza hapa nchini, lakini jukumu kubwa la kuwekeza ni la kwetu, si tu kwenye dawa, lakini hata kwenye bidhaa zingine zozote.

“Hapa tulipo NDC wametuonyesha viwanda mbalimbali, kuna kiwanda cha dawa Kibaha, lakini pia wanataka kufungua kiwanda kingine cha kutengeneza mbao mbadala kule Mafinga na shugjhuli zingine ambazo wanazifanya katika kuchagiza kuendeleza Tanzania ya viwanda,” alisema Dk. Jingu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles