29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Chongolo aanza ziara ya siku Nne Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt,Hai

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chogolo leo Agosti 2, 2022 amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku nne na kuanza kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Wilaya za Hai na Siha.

Mapema baada ya kuwasili Kilimanjaro leo, Chongolo ametembelea kituo cha afya Chekimaji kata Rudugai wilaya ya Hai ambayo itaondoa changamoto ya wanawake wajawazito kutembea umbali mrefu huku wengine wakijifungulia njiani.

Kukamilika kwa kituo hicho cha afya kitahudumia zaidi ya wananchi 14,000 kutoka kata Rudugai na kata jirani za wilaya ya Hai.

Chogolo amesema Serikali imetoa fedha zaidi Sh milion 629 kwa ujenzi wa kituo hicho pamoja na nyumba za wahudumu wa afya katika kituo hicho.

Upande wao wananchi wa Kijiji hicho wameipongeza Serikali kwa kusikia kilio chao cha ukosefu wa huduma za afya kwa muda muda mrefu, hususan kwa wanawake, watoto pamoja na wazee.

Naye mkuu wa divisheni huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe wilaya ya Hai, Etikija Msuya amesema jumla ya fedha zote za mradi wa nyumba za wahudumu wa afya na kituo cha afya zimegharimu Sh million 629.

Msuya ameongeza licha ya mafanikio hayo bado kuna changamoto ya kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles