25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

DK. CHEGENI AANZA MIKAKATI  KUJENGA HOSTELI ZA WASICHANA

Na AHMED MAKONGO-BUSEGA


MBUNGE wa Busega Mkoa wa Simiyu, Dk. Raphael Chegeni (CCM), ametangaza kuanza mikakati ya kujenga hosteli za sekondari kwa wasichana ambao mara nyingi wanakatishwa masomo baada ya kupata ujauzito.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dk. Chegeni alisema uamuzi huo umefikiwa kutokana na kubainika kuwa kati ya wanafunzi 40 wa kike wanaojiunga na kidato cha kwanza wilayani Busega kila mwaka, 15 hadi 18 hukatisha masomo yao kwa sababu ya kupata mimba.

Alisema kukatishwa masomo kwa wanafunzi hao kwa sababu ya ujauzito, hukwamisha ndoto zao hivyo mkakati huo wa kujenga hosteli za wasichana katika shule za pembezoni kutanusuru wanafunzi wengi.

Dk. Chegeni alizitaja shule ambazo zitakuwa katika mpango wa kujengewa hosteli kuwa ni sekondari ya Ngasamo, Imalamate, Mkula, Malili, Kabita na Sogesca ambazo alidai wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu hivyo kupata vishawishi njiani na mwisho ni kupata ujauzito.

Aidha, mbunge huyo alisema kukamilika kwa ujenzi huo kunahitaji fedha nyingi ingawa anayo imani kwamba kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo atafanikiwa.

Wadau hao ni pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Ubalozi wa Ireland, Canada na Serikali kwa ujumla huku akiwataka wananchi  wote kujitokeza kuchangia chochote walichonacho ili kufanikisha mkakati huo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,227FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles