23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko: Ni jukumu la Serikali kuwasikiliza wachimbaji wote wa madini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Madini, Dotto Biteko amekutana na wachimbaji wakubwa wa madini kuwasikiliza na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kodi na usimamizi.

Akizumgumza leo Julai 19, jijini Dar es Salaam alipokutana na wachimbaji hao wakubwa kwenye mkutano wa robo mwaka kusikiliza changamoto, Waziri Biteko amesema Sekta ya Madini imegawanyika kati sehemu kuu tatu wachimbaji wadogowadogo, kati na wakubwa.

Amesema kufanya mkutano huo wa kujadili changamoto ni jambo zuri kwa wadau imezoeleka kuwasikiliza wachimbaji wadogowadogo ni jukumu la Serikali kuwasikiliza wote.

“Leo tunasikiliza na kujadili changamoto mbalimbali za wadau ambao wanachangia kodi lazima tuwasikiliza na changamoto moja wapo ni mwingiliano wa sheria na Wizara ya Maliasili na utalii na Wizara ya Madini lazima tulinde hifadhi na uchimbaji. Na tunajiandaa na mkutano mkuu wa mwaka Oktoba mwaka huu utakunisha wachimbaji na wadau wa madini mbalimbali,” amesema Waziri Biteko.

Amesema asilimia kubwa ya migodini miundombinu imeboreshwa kwaajili ya urahisi wa kufanya biashara kwa wachimbaji hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Faru Ghaphite,Alimiya Othman.

Aidha, Dk. Biteko amesema kwa asilimia Kubwa ajali zimepungua mahali pakazi wachimbaji wanaelewa thamani yao na wanatumia vifaa vya kisasa.

Amesema ifakapo mwaka 2025 kwenye lengo la kuchangia pato la taifa kwa asilimia 10 watakuwa wametimiza lengo na kupitiliza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Faru Ghaphite, Alimiya Othman amesema changamoto zinazowakabili katika mradi mpya uliopo Mkoa wa Morogoro kutoka Ifikara hadi Mahenge umeme na miundombinu.

Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Mines, Mhandisi Philbert Rweyemamu

“Mkutano wa leo tumekutana kutoa taarifa ya robo mwaka wa shughuli wanazofanya wachimbaji wakubwa katika sekta ya madini pamoja na kujadiliana na Serikali namna bora ya kuinua sekta ya madini nchini,”amesema Mhandisi Rweyemamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tembo Nickel, Benedict Busunu amesema Waziri amewashirikisha wadau wakubwa wa madini kukaa pamoja kujadili mustakabali wa sekta hiyo.

“Sisi tumeweza kushiriki kama wadau na kuonesha miradi yetu kwani tumekua tukishirikiana na makampuni makubwa ya madini Duniani ikiwemo BHP hivyo sisi tunaweza kutoa uzoefu wetu katika miradi ya uchimbaji madini,” amesema Busunu.

Mkurugenzi wa Kampuni Tembo Nickel, Benedict Busunu.

Aidha, ameongeza kuwa wanatarajia kwa mara ya kwanza kuanza kuzalisha madini ya Nickel hapa nchini ifikapo kwaka 2026.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles