26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko Mgeni rasmi mkutano wa tatu wa TIA Arusha

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko anataraji kuwa mgeni rasmi kwenye  mkutano wa tatu wa Taasisi  ya Uhasibu Tanzania ( TIA) unaofahamika kama “The Third International Conference on Business Studies”‘ ambao utafanyika jijini Arusha Novemba 7 hadi 9, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa Agosti 7, 2024 na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William  Pallangyo alipotembelea banda la taasisi hiyo lililopo kwenye maonesho ya Kilimo yanayoendelea Viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William  Pallangyo.

Amesema wapo kwenye maonesho  hayo kwa ajili ya kutoa fursa ya elimu kwa wananchi kujua taasisi hiyo majukumu yake pamoja na ushauri wa kitaalamu kwenye nyanja ya kilimo ambapo wamekuwa wakisaidia wakulima, wavuvi na wafugaji kwenye maswala yanayohusu uhasibu kama kuweka kumbukumbu zao za kifedha, kufanya biashara kwa njia sahihi na kupata masoko ya mazao

“Mkutano tumekuwa tunafanya kila mwaka, mwaka huu tunategemea ufanyike  Novemba 7 hadi 9 na mgeni rasmi tunategemea awe ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko atatuongoza kwenye mkutano huo ambao utakuwa na watu wengi na tutakua na washiriki  kutoka sehemu mbalimbali ndani nan je ya nchi,”amesema.

Pia, Prof Pallangyo amesema taasisi yao  imekuwa ikiona changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi hasa za kulipia ada, ambapo amebainisha kuwa kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamepata bahati ya kusoma sekondari lakini wanapofika vyuo vikuu wanapata changamoto za kulipa ada.

Ameeleza kuwa kwa kutambua  hilo TIA imeaandaa “TIA  MARATHON ” lengo likiwa ni kusaidia wanafunzi ambao hawana uwezo wa kifedha.

“Pia mbio za pili zitakuwa ni kwa ajili ya “young mothers” wale wanafunzi ambao wamekuja chuoni lakini pia wana familia , wana watoto wadogo kwa hiyo ili ni kundi ambalo tumeona ni muhimu liweze kusaidiwa kuweza kusoma kwa furaha kwa maana ya kuwasaidia sehemu ya fedha ambazo watazihitaji,” ameeleza.

Ameongeza kuwa  TIA MARATHON inatarajiwa kufanyika Oktoba 26, mwaka huu na mgeni rasmi ni Waziri wa Fedha, Dk.  Mwigulu Nchemba.

Profesa Pallangyo akizungumzia kuhusu kufungua tawi kubwa la TIA  Mkoa wa Tanga amesema ni kati ya mikoa ambayo kwa muda mrefu imekuwa haina taasisi  za elimu ya juu zaidi ungekutana chuo kikuu huria

Aidha, amesema Taasisi yao imefungua tawi letu kubwa Tanga ambalo wanategemea litakuwa linafundisha wanafunzi kuanzia ngazi ya cheti (basic certificate) na Diploma (stashahada) na Serikali imewaruhusu kuanzisha shahada za udhamiri katika campus yao ya Singida, hivyo wananchi walioko karibu na kanda ya kati na maeneo mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles