26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko asisitiza ushirikiano Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Mwandishi Wetu  

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewasisitiza watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya kazi kwa ushirikiano ili  kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

Dk.  Biteko alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati  yeye na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipozungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika kikao kilicholenga   kufahamiana, kujumuika pamoja, kujikumbusha majukumu ya kazi na kufanya tathmini ya utendaji  kazi ili kuongeza ufanisi.

Naibu waziri huyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi wa ofisi hiyo katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali.

“Ninawaomba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mnifundishe, mnielekeze, na kuniombea ili tufanye kazi kwa pamoja kuwahudumia Watanzania na kazi hizo ziwe chachu ya kuboresha maisha ya Watanzania na kupunguza umaskini ,” amesema Dk. Biteko.

Kwa upande wake Waziri  Mkuu Majaliwa, amewataka watumishi hao kuwahudumia Watanzania kwa weledi ili kuisaidia Serikali, kuwa wabunifu katika utendaji kazi, kusimamia Sera ya Uhifadhi wa Mazingira na kuwajibika kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles